Kampuni
ya uchunguzi na utafiti wa madini, Helium One, ambayo kwa sasa inafanya
utafiti wa gesi ya heliamu mkoa wa Rukwa imegundua kuwapo kwa futi za
ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo katika maeneo iliyokwishafanyia
uchunguzi.
Hayo
yalielezwa katika warsha ya siku moja iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar
es salaam, na kuratibiwa na Idara ya Jiolojia ya chuo hicho, Helium One
na Chuo Kikuu cha Oxford.
Akizungumza
katika warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One, Thomas
Abraham-James, alisema kwamba kampuni yao imetafuta leseni 23 za
uchunguzi na kwamba nyingine tatu zimeombwa.
Alisema
kwamba leseni hizo zote zinamilikiwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100
na kwamba ina haki za kipekee za gesi hiyo ya heliamu .
Pamoja
na kutoa taarifa hiyo,alisema lengo la kuwa na warsha ni kuwaita
wataalamu na wadau mbalimbali wa hapa nchini na kimataifa kubadilishana
uzoefu na taarifa zilizopo kuhusu gesi hiyo na kuangalia fursa
zinazoambatana na uwapo wa gesi hiyo katika harakati za kitaifa za kuwa
na taifa la viwanda.
“Helium
One inaamini kwamba kuna fursa kupitia utafiti huu kuweza kutengeneza
utaalamu wa kiwango cha juu na utaalamu wa hapa nchini juu ya
uendelezaji wa gesi hiyo. Tutaendelea kujenga uhusiano na Chuo Kikuu cha
Dar es salaam kuweza kubadilishana elimu, kutoa mafunzo kwa wanafunzi
na maofisa wizara ya madini na kutengeneza mpango wa ufadhili wa
masomo,” alisema.
Kwa
mujibu wa Abraham-James, warsha hiyo ilihudhuriwa na wanasayansi
waandamizi wa gesi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na Idara
ya Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam,UDSM, watu wenye mamlaka na
maamuzi, wadau wa maendeleo, watengeneza sera kutoka serikalini,
watafiti na sekta binafsi.
Aidha
kampuni hiyo imetoa ufadhili wa masomo ngazi ya shahada ya uzamili kwa
wanafunzi wawili wa UDSM kusoma katika Chuo Kikuu cha Oxford , ikiwa ni
sehemu ya kuingiza utaalamu wa hali ya juu wa kisayansi kwa watanzania
na pia kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Helium One na UDSM.
Wakati
wa warsha hiyo, Profesa John Machiwa, akimwakilisha Makamu Mkuu wa
Chuo, Prof Cuthbert Kimambo, alisema kwamba jukwaa hilo ni jema kwa
wanafunzi, wakufunzi na Chuo kizima kutafuta njia ya kuona namna ya
kushirikiana na Helium One.
“Tunaweza
kufanyakazi pamoja na kunoa taaluma na pia kupata utaalamu katika
utafiti wa heliamu uzalishaji na usafirishaji wake,” alisema.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment