Wednesday, 24 January 2018

Msongo wa Mawazo Husababisha Unene?

Sote tunafahamu nini kinatufanya tunenepe: ulaji wa vyakula vyenye kalori kupita kiasi.

Japo jibu hili ni la kweli, halijibu swali la msingi zaidi - je, ni kwanini watu hula chakula kupita kiasi?

Ni kwa nini wakati mwengine najihisi kula keki ama chokleti licha ya kwamba nafahamu nitajutia baada ya dakika chache zijazo?

Kwa mara nyingi huwa ni tamaa - ama ni kitu chengine kinachoendelea?

Licha ya kwamba nidhamu ni muhimu, kuna ushaidi mwingi kwamba msongo wa mawazo huchangia pakubwa kwa mtu kuongeza kilo za mwili.

Msongo wa mawazo kupita kiasi, huathiri jinsi mtu anavyopata usingizi na viwango vya sukari mwilini. Hali hiyo huongeza njaa na kuzidisha zaidi ulaji wa chakula kwa utaratibu.

Na hali hiyo huathiri zaidi usingizi, hata viwango vikubwa vya msongo wa mawazo huathiri zaidi viwango vya sukari. Kwa muda, huo unaweza kusababisha viwango vikubwa vya mafuta na kisukari aina ya type -2.

Na kuona kile kinachoweza kutokea, Dkt Giles Yeo, mwanachama wa Trust Me ,yeye ndiye daktari wa timu ambayo pamoja na usaidizi wa wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Leeds, aliamua kujiweka yeye mwenyewe kwenye katika hali ngumu ya msongo wa mawazo.

Wanasayansi wa Leeds walianza kwa kumuuliza Giles kufanya mambo tofauti ambayo yangemsababishia msongo wa kiakili.

Walimuweka mbele ya tarakilishi na wakamlazimisha kufanya hesabu ya kuondoa ,17 , kutoka kwa nambari kama 2,043. Na alipokuwa akikosea, waliona akipatwa na hali ya msongo wa mawazo jambo ambalo lilimpatia Giles shida.

Baada ya hapo wakamlazimu kuweka mikono yake kwenye beseni ya maji baridi kwa muda. Kabla na baada ya uchunguzi huo, kikosi hicho cha chuo kikuu cha Leeds wakampima kiwango cha sukari.

Kiwango cha sukari mwilini huongezeka wakati mtu anapokula, na kwa mwenye afya njema kama Giles, kiwango hicho cha sukari hushuka na kuwa kawaida kwa haraka.

Lakini kikosi hicho cha Leeds kilibaini kwamba siku ambayo Giles alikuwa amepitishwa kwenye shida hizo zote, bado kiwango cha sukari kilichukua muda wa saa tatu kurudi katika hali ya kawaida ambayo ni mara sita zaidi katika siku ambayo mtu ametulia bila wasiwasi wowote.

Sababu kuu ambayo husababisha hayo ni kwamba endapo mtu anapata msongo wa mawazo, mwili hujipata ''ukipigana.''

Mwili hudhani uko katika mashambulizi na hutoa glukosi kwenye damu ili kuongeza nguvu kwenye misuli.

Lakini endapo huhitaji nguvu za kukimbia kujiepusha na hatari yoyote ile, basi wengi hutoa insulini ili kuweza kurudisha kiwango cha sukari kwa kiwango cha kawaida.

Ongezeko la kiwango cha insulini na kushukwa kwa kiwango cha sukari humfanya binadamu kuhisi njaa na ndio sababu kuu kumfanya mtu kutamani kula vyakula vya sukari hasa iwapo mtu anakumbana na msongo wa mawazo.

Kitu kama hicho hutokea iwapo hujapata usingizi mzuri usiku. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na watafiti wa chuo kikuu cha King, mjini London imebaini kwamba iwapo mtu akikosa usingizi anauwezo wa kula zaidi ya kalori 385 kwa siku , ambayo ni sawa na kalori iliyoko kwenye keki ndogo.

Watoto pia hupata tamaa ya vyakula vya sukari iwapo hawajalala vizuri, kwenye utafiti mwengine,wa hivi karibuni, watafiti walichukua kikundi kidogo cha watoto wenye umri wa miaka mitatu na minne ambao hulala kila siku mchana na kuwalazimu kutolala mchana mmoja na kuhakikisha wamekaa macho saa mbili zaidi wakati wao wa kwenda kulala kila siku.

Usingizi ni muhimu kwa binadamuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Usingizi ni muhimu kwa binadamu
Siku ya pili ,watoto hao walibugia asilimia 20 ya kalori kuliko kawaida, hasa vyakula vyenye sukari nyingi na waliruhisiwa kulala kwa muda waliotaka.

Na siku ya tatu, bado watoto hao walikula kalori asilimia 14 kuliko kawaida.

Jinsi za kupunguza msongo wa mawazo kila siku?

Kitu cha kwanza, ningependa watu wanashauriwa kupata usingizi wa kutosha. Hili ni rahisi kwa kusema na si kwa vitendo, lakini mamlaka ya huduma ya afya-NHS inatupatia mbinu muhimu za kufuata.

Pia ungejaribu njia ambazo zinazofahamika zinazopunguza msongo wa mawazo kama vile mazoezi, ukulima ama kushiriki mazoezi ya yoga.

Lakini kitu muhimu tulichobaini kwenye utafiti wetu ni kwamba utafaidika iwapo ulifurahia.

Kwa hivyo jaribu kufanya vitu tofauti na uone kile kinachoweza kukufaa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment