Home »
Habari Moto
» Jeshi la PolisiYadai Nabii Tito Ana Matatizo ya Akili Apelekwa Kupimwa Milembe.
JESHI la Polisi mkoani Dodoma, baada ya kumkamata na kumfanyia mahojiano Onesmo Machija (44) anayejiita ‘nabii’ Tito, kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya, limesema mtu huyo ana matatizo ya akili. Akizungumza na wanahabari mjini Dodoma leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gillesi Muroto, amesema mnamo Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba baada ya hapo, Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.Kwa msingi huo, alisema jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Mirembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dkt. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo.Pamoja na hayo, Muroto alisema jeshi la polisi mkoani humo bado linaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
#BREAKING NEWS>>WATU WANAO DHANIWA NI POLISI WAVAMIA NYUMBA YA GWAJIMA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Watu
wanaodhaniwa kuwa ni polisi wamezingira Nyumba ya Askofu Mkuu wa
Makanisa ya Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima huko Salasala muda huu.
Bado haijafahamika wanatafuta nini.
Download Application ya Heb… Read More
HEKAHEKA: Mtoto mchanga aliyeibwa Tegeta apatikana Makaburini Ununio.Fahamu zaidi hapa.
February 22 2017 kupitia Leo Tena ya Clouds FM Heka Heka ilitokea Tegeta Kibaoni Dar es salaam ambapo Mtoto mchanga aliibwa na watu ambao hawakufaamika..Sasa Leo February 28 zikiwa zimepita siku si… Read More
Waziri Nape: Sikupinga vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya bali nilishauri busara itumike.Fahamu zaidi hapa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi
juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa
za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.… Read More
Waziri Nape: Nitajiuzulu Uwaziri Kama Itabainika Natoka Kimapenzi na Wema Sepetu.Fahamu zaidi hapa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atajiuzulu
uwaziri endapo mtu atampelekea ushahidi wa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na msanii yeyote.
Kauli
hiyo ya Nape inakuja ikiwa ni takriban … Read More
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afungua mkutano wa watendaji Wakuu wa Mashirika ya umma,Ikulu.Fahamu zaidi hapa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa mapema leo 28 Februari 2017, ameongoza mkutano
wa siku moja wa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi za mashirika ya
umma, unaojadili nafasi za mashirika ya Umma katika utekelezaj… Read More
0 comments:
Post a Comment