Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa gharama mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki itakuwa Sh. 150,000.
Dk Nchemba amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam ambapo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha Dkt. Miwgulu Nchemba amesema kuwa Pasipoti hizo zitakuwa na ukurasa zaidi ya mmoja na mwonekano mpya.
“kiasi cha gharama hiyo ni sawa na Sh15,000 kwa mwaka kwa sababu itatumika kwa miaka 10. Gharama za kupata pasipoti sasa ni TSh.50,000 na hutumika kwa miaka 10 tangu zilipotolewa,“ amesema Dkt. Mwigulu.
Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa gharama ya laki moja na nusu bei hiyo ni ya juu kidogo kuliko bei ya sasa . huku kieleza kuwa bei hiyo imezingatia ubora wa utenngenezaji wa Pasipoti hiyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment