Sunday, 2 August 2015

Jionee ubunifu hapa.
















#YALIYOJIRI>>>> Chama cha wafanyakazi madereva Tanzania(TADWU) kimetangaza mgomo wa madereva nchi nzima kuanzia Agosti tisa mwaka huu




Chama cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU- kimetangaza mgomo wa madereva nchi nzima kuanzia Agosti tisa mwaka huu baada ya wamiliki wa mabasi, wakala wa usafiri wa nchi kavu na majini pamoja na wizara ya kazi kushindwa kutekeleza makubaliano yalifikiwa na tume iliyoundwa na waziri mkuu kutatua mgogoro wa madereva nchni.
Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana Rashidi Salehe wakati akizungumza na wahandishi wa habari ambapo amesema mgomo huo unarejea tena baada ya wamiliki wa mabasi kwa kushirikiana na wizara kazi pamoja na Sumatra kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni wakati makubaliano ya tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya ianze kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.

Wakizungumza na wahandishi wa habari baadhi ya madereva wamelalamikia wizara ya kazi na sumatra kwa kukaidi agizo la waziri mkuu na kuendelea kupokea mikataba ya zamani toka kwa wamiliki wa mabasi na kutoa leseni wakati makubaliano yalishafanyika na kusisitiza katika makubaliano hayo mishahara ya madereva wa malori yanayotoka nje ya nchi walikuwa wanatakiwa kulipwa mishahara ya shilingi milioni moja, huku madereva wa daladala shilingi laki tano pamoja na posho nyingine.

Akizungumza kwa simu na mmoja wa viongozi wa chama cha wamiliki wa mabasi nchni kwa masharti ya kutotajwa jina amewalalamikia madereva hao kwa kupanga mgomo badala ya kupeleka madai yao kwa tume ya kudumu iliyoundwa na waziri mkuu ili kupata ufumbuzi ambapo amesema kuna baadhi ya madereva wanatengeneza migomo ili kuleta usumbufu kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

#YALIYOJIRI>>>>Timu ya Azam yachukua kombe leo la Kagame bila kufungwa.




Azam FC imeweka historia baada ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza ikiwa ni timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa kombe hilo.
Lakini historia ya kuvutia zaidi ni kutwaa ubingwa wa kimataifa wa CECAFA Kagame Cup kwa kucheza mechi sita za mashindano na timu mabingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja.
Uongozi wa Azam FC umethibitisha kwa vitendo kuwa haukukosea kumrejesha Kocha Muingereza Stewart Hall klabuni baada ya kukaa nje ya klabu kwa miezi 13 kwani miezi miwili tuu baada ya kutua amewezesha klabu kutwaa kikombe kikubwa baada ya kuwachapa Gor Mahia ya Kenya bao 2-0.
Mabao hayo yaliyowapa heshima Azam FC yalipachikwa dakika ya 16 na nahodha John Bocco (Boko Haram) aliyeunganisha krosi safi ya Muivory Coast Kipre Tchetche na la pili lilimaliziwa na Tchetche dakika ya 65 kwa njia ya faulo iliyokwenda moja kwa moja golini na kumshinda kipa wa Gor Boniface Oluoch.
Katika mchezo huo, Azam FC ilicheza soka la mbinu za ushindi ikitumia fomesheni ya 3-5-2 waliipoteza kabisa Gor Mahia hasa washambiliaji wake Meddy Kagare na Michal Olunga ambao hawakufulukuta kwa ngome iliyoongozwa na Serge Wawa Pascal.
Azam FC ilifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa, Ame Ally na kumwingiza Frank Domayo dakika 46 Farid Mussa akaingia Erasto Nyonni na Tcxhetche alitoka akaingia Didier Kavumbagu dakika ya 86
Azam FC pia imeweka historia ya aina yake baada ya wachezaji wake kushinda tuzi za mchezaji bora kila mechi. beki wa kati, Muivory Coast, Serge Wawa 'Waziri wa Ulinzi' amekuwa mchezaji bora wa mechi tatu huku Salum Abubakar, Farid Mussa Shah na Aishi Salum Manula wakishinda tuzo hiyo mara moja kila mmoja. Kwa maana hiyo wachezaji wa Azam FC walishinda tuzo za mchezaji bora wa mechi kwenye kila mchezo.
Kivutio kingine ni kwa Serge Wawa Pascal kuwa mchezaji bora wa mashindano huku mlinda lango Aishi Manula akishinda tuzo ya nyanda bora wa mashindano.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Said Morrad,Aggrey Morris, Serge Wawa, Mugiraneza Jean Baptiste, Himid Mao, Kipre Tchetche/Kavumbagu, Ame Ally/Frank Domayo, Bocco, Farid Mussa/ Erasto Nyoni.
     Chanzo 
                    Azam FC.

Saturday, 1 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Sikiliza Audio ya Nuhu Mziwanda akimtongoza Wema Sepetu hapa.

Hii audio inaweza ikawa imevuja wakati mmbaya sana hasa ukizingatia ni kipindi ambacho mpenzi wake Nuh mziwanda, Shilole yupo kwenye matatizo ya kufungiwa kujihusisha na kazi yoyote ya kisanaa. Audio hiyo inaoneshwa ni ya muda kidogo kwasababu Wema anasikika akizungumzia kwenda kwenye KTMA.
Toa maoni yako hapa chini.

#YALIYOJIRI>>>Mapokezi ya Diamond Platnumz huko Kenya yajaza watu wengi.





Msanii wa kizazi kipya anafaa mika kwa ji Diamond Platnumz amewasili NAIROBI akikuta mapokezi makubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomokinyata  huku akizungukwa na wahandishi wa habari na mashabiki wake.




Jifunze kuwa desiger hapa.
















Haya yote yanapatikana kwenye page zangu zote.