Chama
cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU- kimetangaza mgomo wa madereva nchi
nzima kuanzia Agosti tisa mwaka huu baada ya wamiliki wa mabasi, wakala wa
usafiri wa nchi kavu na majini pamoja na wizara ya kazi kushindwa kutekeleza
makubaliano yalifikiwa na tume iliyoundwa na waziri mkuu kutatua mgogoro wa
madereva nchni.
Kauli
hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana Rashidi Salehe wakati
akizungumza na wahandishi wa habari ambapo amesema mgomo huo unarejea tena
baada ya wamiliki wa mabasi kwa kushirikiana na wizara kazi pamoja na Sumatra
kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni wakati makubaliano ya
tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya ianze kutumika kuanzia
julai mosi mwaka huu.
Wakizungumza
na wahandishi wa habari baadhi ya madereva wamelalamikia wizara ya kazi na
sumatra kwa kukaidi agizo la waziri mkuu na kuendelea kupokea mikataba ya
zamani toka kwa wamiliki wa mabasi na kutoa leseni wakati makubaliano
yalishafanyika na kusisitiza katika makubaliano hayo mishahara ya madereva wa
malori yanayotoka nje ya nchi walikuwa wanatakiwa kulipwa mishahara ya shilingi
milioni moja, huku madereva wa daladala shilingi laki tano pamoja na posho
nyingine.
Akizungumza
kwa simu na mmoja wa viongozi wa chama cha wamiliki wa mabasi nchni kwa
masharti ya kutotajwa jina amewalalamikia madereva hao kwa kupanga mgomo badala
ya kupeleka madai yao kwa tume ya kudumu iliyoundwa na waziri mkuu ili kupata
ufumbuzi ambapo amesema kuna baadhi ya madereva wanatengeneza migomo ili kuleta
usumbufu kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment