Thursday, 29 December 2016

TOFAUTI 7 Kati ya Mume Mwenye Mke Mmoja na Mwenye Mke zaidi ya Mmoja.Fahamu zaidi hapa.

1. Mume mwenye mke mmoja huwa hana uwezo mkubwa wa kufanya tendo la ndoa, wakati mwenye mke zaidi ya mmoja huongezeka nguvu za kufanya tendo la ndoa maradufu.
(N.B ...mwanaume anapofanya tendo mara kwa mara nguvu na uwezo wa tendo hilo huongezeka na joto la mwili pia, wakati mwanamke anapo fanya tendo mara kwa mara hupoteza hamu ya penzi na afya pia)

2. Mume mwenye mke zaidi ya mmoja huwa hana tatizo la kupata likizo (kumsaidia mke kuingia siku zake) bali kama mke mmoja yupo likizo huweza kukidhi matamanio kupitia mke wa pili, tatu au nne)

3. Mume mwenye mke zaidi ya mmoja kuwa na upeo mkubwa zaidi wa fikra na ufaham kuliko mwanaume mwenye mke mmoja. (N.B ...kama una mke mmoja na una upeo mkubwa basi endapo utaongeza mke utakuwa na upeo na ufahamu mkubwa zaidi ya huo ulionao sasa kwani pia utakuwa na washauri zaidi ya mmoja.)

4. Mume mwenye mke zaidi ya mmoja huwa na mafasi ya kubembelezwa na kuheshimiwa ndani na nje ya familia kuliko mume mwenye mke mmoja.(N.B.. hii hutokana na maumbile waliyoumbwa wanawake ya kushindana kwenye kuonyesha mapenzi kati yao hasa anapo jua kuna anae weza kuipokonya nafasi yake ya kupendwa zaidi.)

5. Mume mwenye mke zaidi ya mmoja huwa anajiamini(confidence) zaidi kuliko mume mwenye mke mmoja. kuthibitisha hilo ndio maana akathubutu kuongeza mke wa pili, tatu au nne.

6. Mume mwenye mke zaidi ya mmoja hufurahikia tendo la ndoa tena kwa utam zaidi kuliko mwenye mke mmoja. (N.B... mwanamke anapokaa mda mrefu bila kufanya jimai joto la mwili wake huwa la juu zaidi na mihemko ya kutamani tendo hilo la ndoa huzidi, hii huongeza ladha zaidi kwa wote.)

7. Mume mwenye mke zaidi ya mmoja huwa na DARJA ya juu zaidi katika mizani ya familia kuliko mwenye mke mmoja.

N.B:
UCHUNGUZI WA KISAYANSI UMEZINGATIWA ZAIDI.
**

Imeandaliwa na IKA MATRIMONIAL AND COUNSELLING SERVICES.
kwa ushauri wa ndoa na familia:


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

MITANDAO ya Kijamii Hatari zaidi Kuongeza Ugaidi.Fahamu zaidi hapa.

Vikundi vya kigaidi vinatumia aina zote mpya za mitandao ya kijamii na teknolojia ya mawasiliano ili kupanua wigo wa mitandao yao sambamba na kufadhili shughuli zao.

Hiyo ni kwa mujibu mwakilishi wa kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi, Delphine Schantz ambapo amesema tovuti na majukwaa mbali mbali kwenye mitandao hiyo inatumika kuchangisha fedha na kununua silaha kupitia kwenye mitandao.

Aidha ameongeza kuwa juhudi za pamoja zahitajika kufuatilia mifumo hiyo kwa kuwa Hakuna nchi mwanachama ambayo ni salama dhidi ya ugaidi au salama dhidi ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya ugaidi.

Bi. Schantz amesema kamati yao hivi sasa inafuatilia tovuti zinazohusika na uandikishaji magaidi na uchangishaji fedha lakini jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wana uelewa wa kutosha kuwa mitandao hiyo inaweza kutumika vibaya kueneza ujumbe mbaya wa kuchangisha fedha kwa ajili ya ugaidi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

KADA WA CHADEMA ataka Mhe.Kubenea akamatwe na polisi ni baada ya kudai BEN SAANANE amejificha kwa marafiki zake.Fahamu zaidi hapa.

 
by Malisa GJ
Taarifa za Mhe.Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni
taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?
 
Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?
 
Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?
 
Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?
 
Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.
 
Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).
 
Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!
 

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi.Fahamu zaidi hapa.

Bondia Francis Cheka ametangaza rasmi kuachana na mchezo wa ngumi na kujielekeza kwenye masuala binafsi ya kibiashara.
Mwanandondi huyo kutoka Morogoro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa ITV mjini Morogoro kuhusu taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii vikimhusiha na utapeli wa kukimbia ulingoni Dec 25 mwaka huu huko jijini Dar es Salaam, alikotakiwa kupigana na bondia Dula Mbabe,ambapo amebainisha kutofika ulingoni siku hiyo hakukumaanisha kuhofia pambano hilo bali ni kutokana na promota wake Kaike Selagi kutomlipa fedha zake zote kama walivyokubaliana, ambapo amedai alipaswa kulipwa milioni tisa, lakini hadi wanamaliza kupima uzito alikua amepewa milioni tatu pekee.

Akizungumzia azma ya kuachana na ngumi,Cheka amesema kwa muda mrefu amekuwa akipigana bila mafanikio kutokana na kudhulumiwa na waandaaji au kulipwa tofauti na makubaliano sambamba na misukosuko ya hapa na pale anayofanyiwa na wapinzani wake na kwamba anaamini wapo baadhi ya watu waliolenga kumshusha kwenye ngumi badala ya kumtengeneza bondia mwingine mwenye uwezo na kumpiga na kwamba kwa sasa atajielekeza kufanya biashara zake na kuahidi ushirikiano kwenye mchezo wa ngumi ili kukuza na kuendeleza mchezo huo.

Source: ITV

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Mke wa anayedaiwa kutobolewa macho na ‘Scorpion’ atoa ushahidi Mahakamani.Fahamu zaidi hapa.

Stara Sudi, mke wa Saidi Mrisho ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jinsi alivyoshtuka baada ya kupokea simu aliyopiga mumewe kuwa amevamiwa na kuchomwa visu machoni, mgongoni na tumboni. 
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Salum Njwete (34) maarufu ‘Scropion’, Stara alimueleza Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa Septemba 6, saa tano usiku akiwa amelala alipokea simu yenye sauti ya mumewe ikieleza kuwa amevamiwa. 
“Aliniambia mama Nancy nimechomwa visu hata kuona sioni hapa nilipo nipo Buguruni,” alidai Stara ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa mashtaka. 
Alidai tangu wafunge ndoa na mumewe Oktoba 2015 , Said alikuwa akifanya kazi ya kinyozi katika saluni ya Rodgers iliyopo Tabata Sanene. 
“Baada ya kuongea na mume wangu, simu ilikatika lakini wakati natafuta nguo nivae simu ileile ilipiga na nilipopokea sauti ya mtu mwingine iliongea ambaye ndiye mwenye simu na aliniambia kuwa mume wangu ana hali mbaya hivyo nifanye haraka niende Hospitali ya Amana,” alidai Stara. 
Baada ya kupata taarifa hizo, alidai alimweleza mtoto wao mkubwa, Abdul Said (12) kuwa anaelekea Amana. Lakini kabla ya kwenda huko alichukua pikipiki na kwenda Mabibo Hosteli anakoishi mama mkwe wake kumweleza taarifa hiyo na kwamba waliambatana hadi Amana. 
Alidai wakiwa njiani, walimjulisha mdogo wa Saidi, Yahaya Kisukari (23) kuwa kaka yako amepata matatizo ya kuvamiwa na mtu akachomwa visu na yupo Hospitali ya Amana. 
“Tulipofika Amana, tuliruhusiwa kuingia wodini na kumuona mume wangu akiwa amefungwa bandeji machoni na sehemu nyingine za mwili, huku damu ikivuja sehemu mbalimbali za mwili. Hata nguo aliyovaa ilikuwa imejaa damu,” aliiambia Mahakama na kuongeza: “Baada ya kumvua nguo zilizo- kuwa zimetapakaa damu, tulipewa rufaa kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu na wakati huo ilikuwa imeshafika saa sita usiku.” 
Stara alidai baada ya kumuona mumewe aliyechomwa visu na mtu aliyemtaja kwa jina la Scorpion, alikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Buguruni. 
“Baada ya kutoa maelezo Polisi Buguruni na askari kwenda kuchukua maelezo ya mume wangu Muhimbili, tulikwenda kumkamata mshtakiwa Salum Njwete,” alidai. 
Alidai: “Septemba 8, tulirudi tena Muhimbili na kupewa taarifa na daktari wa macho aliyemfanyia upasuaji Said kuwa macho yake hayataona tena.” Stara alidai tangu waoane na mumewe, hajawahi kupata malalamiko yoyote kuwa mwenza wake huyo ni mwizi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Wednesday, 28 December 2016

#BREAKING NEWS>>>Azamfc watimua benchi lote la ufundi leo hii.Fahamu zaidi hapa.

  Azam FC imeamua kuwatimua makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.

Uamuzi wa Azam umekuja baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu tangu ‘wahispaniola’ walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya Stewart Hall kubwaga manyanga.

“Uongozi wa Azam FC umewatimua makocha wao leo mchana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili,” chanzo cha kuaminika toka ndani ya Azam FC kimeiambia shaffihdauda.co.tz.

Katika mechi 17 za VPL ambazo Hernandez alisimama kama kocha mkuu wa Azam FC, timu hiyo imeshinda mechi saba (7), imetoka sare mara sita (6) na kupoteza michezo minne (4).

Hadi sasa Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17. Azam inazidiwa pointi 14 na Simba ambao ndio vinara wa ligi huku wakiwa nyuma kwa pointi 10 dhidi ya Yanga huku wakizidiwa pointi moja na Kagera Sugar.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi



Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

MWINGEREZA CLATTENBURG ATANGAZWA KUWA MWAMUZI BORA DUNIANI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mark Clattenburg ametangazwa kuwa mwamuzi bora zaidi duniani baada ya kushinda tuzo maarufu kwa jina la Globe Soccer Awards.

Mwaka 2016 umekuwa ni wenye mafanikio kwa mwamuzi huyo Mwingereza.

Ndiye alicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyohusisha timu zote za Hispania zinazotoka kwenye mji mmoja za Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid.

Pia alichezesha fainali ya Kombe la FA wakati zilipokutana Crystal Palace dhidi ya Manchester United iliyobeba ubingwa.

27

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

LIVERPOOL MWENDO WA KASI, YAIBAMIZA 4-1 STOKE CITY.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mshambuliaji wa Kibrazil, Roberto Firmino akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili dakika ya 44 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Stoke City Uwanja wa Anfield leo. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Goals: Adam Lallana dakika ya 34, Giannelli Imbula aliyejifunga dakika ya 59 na Daniel Sturridge dakika ya 70, wakati bao la Stoke City limefungwa na Jon Walters dakika ya 12.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Ngoma apatia goli timu yake ya Yanga.Fahamu zaidi hapa.

Afanya yake Ngomaaaaaa goooooo dk 4

Endelea kufatilia hii blog "www.hebronmalele.blogspot.com"

 kwa habari zaidi za michezo.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK YAGONGA MTU 2-0.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi jana na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.


Genk ilikuwa inacheza kwa mara ya kwanza leo bila ya kocha wake Mbelgiji Peter Maes iliyemfukuza jana na ikafanikiwa kushinda.


Samatta aliingia dakika ya 51 kwenda kuchukuaa nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelisn wakati huo tayari Genk inaongoza 2-0 mabao ya Pozuelo dakika ya 19 na Karelis kwa penalti dakika ya 26.

Maes ndiye aliyemsajili Samatta Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na akamuamini haraka na kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.


jana Samatta amecheza mechi ya 36 Genk,18 msimu uliopita na 18 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu.


Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na matano msimu uliopita.


Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Ndidi, Heynen, Pozuelo/Susic dk89, Bailey/Trossard dk81, Buffalo and Karelis/Samatta dk51.AA Gent : Rinne, Neto, Mitrovic Saief/Verstraete dk66, Nielsen/Desmet dk66, Perbet, Simon Foket, Esiti. Dejaegere) Gershon and Milicevic.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Darasa aiteka ILALA DAR baada ya kufanya show mchana wa leo.Fahamu zaidi hapa.


DARASA AISIMAMISHA ILALA KWA SHOO KALI
MWANAMUZIKI wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.

Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.

Akizungumza na mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.”

Naye Meneja wa Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo.”

Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”

Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

HAWA NDO WASANII WA BONGO WALIO POTEZWA NA MADAWA YA KULEYVA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MDADA ALIYE JIINGIZA KATIKA MADAWA YA KULEVYA NA KUPELEKEA KUHARIBU NDOTO ZAKE ZOTE KIMUZIKI NA MAISHA KWA UJUMLA

CHIDY BENZ
NI MSANII WA HIP-HOP ALIYE TOKEA LUPENDWA SANA HAPA TANZANIA …SASA KAJIINGIZA KATIKA MADAWA YA KULEVYA JAPOKUWA ALISAIDIWA NA BABU TALE ILA YAONYESHA KARUDIA TENA NA KHALI YAKE KWA SASA NI MBAYA SANA

LOYD EYES
 KIJANA WA KIARUSHA TOKA KUNDI LA WEUSI ,ALIONDOLEWA KATIKA KUNDI KUTOKANA NA TABIA ZAKE ZA MADAWA YA KULEVYA ,RAY C ALIMSHUTUMU KUWA YEYE NDIYO CHANZO CHA KUMFANYA RAY C ATUMIE MADAWA YA KULEVYA ..HUKU YEYE AKIJITAHIDI KURUDI KIMUZIKI,WENZAKE NDO WAKO JUU KWA SASA NA WASHAPENYA HADI ANGA ZA KIMATAIFA.

YOUNG D
MTOTO MDOGO AMBAYE AMEATHILIWA NA MAKUNDI ANAYO AMBATANA NAYO PIA KUIGA MAISHA YA WASANII WA NJE NDIKO KULIKO MPELEKEA YOUNG D MSANII MWENYE KIPAJI KIKUBWA KUJIINGIZA KATIKA KUNDI LA WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA NA KUFANYA KUPOROMOKA KIMUZIKI KWA KIASI KIKUBWA.

FANANI
HUYU NI MOJA YA WAKONGWE WA MUZIKI WA BONGO AKITOKEA KATIKA KUNDI LA HBC AKIWA PAMOJA NA PROFESSOR J AMBAYE KWA SASA NI MBUNGE WA MIKUMI.FANANI MWENYE KIPAJI KIKUBWA ALIJIINGIZA KATIKA MADAWA YA KULEVYA NA KUPELEKEA KUHARIBU NDOTO ZAKE ZOTE ZA MAISHA KIUJUMLA.

DAZ BABA
MSANII TOKA KUNDI LA DAZ NUNDAZ ALIYEWIKA NA NGOMA YA UMBO NAMBA NANE ENZI HIZO NA KUWEZA KUTEKA KABISA TASNIA YA BONGO FLEVA TANZANIA NZIMA ,LEO HII NAYE KHALI YAKE SIO NZURI KUTOKANA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA

20 PERCENT
HUYU NI MSHINDI WA TUZO 5 ZA KILIMANJARO KUTOKANA NA UIMARA WAKE KATIKA UTUNGAJI PIA KATIKA KUIMBA NYIMBO ZENYE UJUMBE MZITO KWA JAMII,LEO HII KAPOTEA KABISA KUTOKANA NA MADAWA YA KULEVYA.

FEROOZ
FEROOZ MSANII ALIYEWEZA KUPEWA ZAWADI YA GARI NA MHESHIMIWA RAIS WA AWAMU YA TATU MKAPA KUTOKANA NA UIMARA WAKE WA KUIMBA NYIMBO YA UKIMWI AKIMSHIRIKISHA PROFESSOR J.HAKIKA NI MTU AMBAYE HAKUJIPANGA IPASAVYO LEO HII ILIBIDI AWE NI MTU MWENYE MALI ZAIDI HATA YA DIAMOND LAKINI KUTOKANA NA KUTO ANGALIA MBALI LEO HII FEROOZ NI MTU AMBAYE UKIMUONA HUWEZI AMINI HAKIKA MADAWA HAYAFAI KATIKA JAMII.

KR
KR MULLAR MWANZILISHI WA STYLE YA MAPANGA KATIKA UCHEZAJI,LEO HII KR NI MTU WA KUMUONEA HURUMA KUTOKANA NA JINI ALIVYO CHEZEA NAFASI ALIYO KUWA NAYO KIPINDI KILE ,MADAWA YA KULEVYA YASEMEKANA KUWA CHANZO CHA YOTE HAYA.HIVI JUZI PICHA ZAKE ZILISAMBAA ZIKIONYESHA AKIWA KALEWA HAJITAMBUI MCHANA KWEUPEE.
Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

KIKOSI CHA YANGA KINACHOSHUKA UWANJANI LEO KUIVAA NDANDA HIKI HAPA.

Yanga ipo uwanjani leo Jumatano, itakipiga dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kushuka uwanjani leo hiki hapa:
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Vicent Bossou
5. Kelvin Yondani
6. Said Juma
7. Simoni Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Amisi Tambwe
11. Emanuel Martin

Wanaoanzia benchi
Ali Mustafa
Andrew Vicent
Justin Zullu
Thabani Kamusoko
Obrey Chirwa
Geofrey Mwashuiya
Deusi Kaseke.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Haya ndio majibu ya mchezaji wa Simba, Ibrahim Hajib baada ya kufanya majiribio Misri.Fahamu zaidi hapa.

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Ibrahim Hajib ambaye hivi karibuni alienda Nchini Misri kufanya majaribio katika klabu ya Haras El Hodoud ya Ligi Kuu ya Misri.
Hajib (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Haras El Hodoud mazoezini leo mjini Alexandria
Hajib akiongea na Bin Zubeiry Sports kutoka mjini Alexandria yalipo makao makuu ya timu hiyo, Hajib alisema kwamba ameambiwa amefuzu majaribio yake baada ya siku tano.
“Nimepewa majibu kwamba nimefuzu, kwa hiyo kinachofuata ni hii klabu kuzungumza na Simba ili wakubaliane kwanza, ndipo nitajua mustakabali wangu,”amesema Hajib.
Hajib ambaye aliondoka Alhamisi iliyopita nchini kwenda Misri kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa baada ya kupewa baraka zote na uongozi wa Simba.
Source: Bin Zubeiry Sports

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

VIDEO:Mashabiki Wadai Fedha zao Baada ya Ali Kiba Kushindwa Kufanya Show Dodoma.Fahamu zaidi hapa.

Disemba 25, ikiwa ni sikukuu ya Krismasi mashabiki wa mwanamuziki Ali Kiba walibaki wakiwa wamepigwa butwaa bila kuona mtu jukwaani huku muda ukiyoyoma katika tamasha la muziki ambalo Ali Kiba alitakiwa kutumbuiza siku hiyo.

Hadi inafika saa saba usiku mwanamuziki hiyo hakuwepo ukumbini alipotakiwa kuanza kutumbuiza saa nne. Baadhi ya watu waliokuwa ndani ya ukumbi walianza kuleta vurugu na kudai fedha zao ili waondoke kwani muda ulikuwa umekwenda sana.

Akizungumza, mtayarishaji wa tamasha hilo Rashid Adam maarufu Chidi Perugina alisema tatizo kubwa lilikuwa ni suala la usafiri ambapo Ali Kiba alichelewa kufika mkoani Dodoma.

Ali Kiba alikuwa Nairobi na alitegema apande ndege awahi kufika Dar es Salaam na kisha aanze safari ya kuja Dodoma, lakini tatizo lilitokea baada ya Ali Kiba kukosa ndege ya kwanza aliyotakiwa kutoka nayo Nairobi. Ndege ya pili aliyopanda ilichelewa kufika Dar es Salaam na kuanza mchakato wa safari ya kufika Dodoma ulisababisha Ali Kiba kufika hapa saa saba usiku na madakika, alisema Rashid Adam.

Baada ya Ali Kiba kufika aliwaomba radhi mashabiki wake wachache waliokuwa bado wapo ukumbini na hakuweza kutumbuiza sababu ya uchache wao.


Baada ya tamasha hilo kusindwa kufanyika hiyo tarehe 25 Disemba, Ali Kiba anatarajiwa kutumbuiza terehe 28, Januari 2017 ambapo mashabiki walio na tiketi wametakiwa kuzitunza ili kuzitumia kwenye tamasha hilo lingine. Angalia Video: 


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

#BREAKING NEWS>>>Dhamana ya Mbunge Lema yakwaa kisiki mahakamani, arejeshwa rumande.Fahamu zaidi hapa.

Mbunge Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.

Rufaa hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.

Upande wa mtuhumiwa uliongezea muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda uliokuwa umepangwa awali.

Mbunge Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Yafahamu matunda ambayo hupunguza maumivu makali wakati wa hedhi.Fahamu zaidi hapa.

Mzunguko wa hedhi ni mzunguko wa kila mwezi ambao mwanamke huupata, hali ambayo huleta kutokwa na damu ukeni kutokana na mimba kutotungwa. Kwa hali ya kawaida hedhi ya kwanza hutokea katika umri wa miaka 12 -13 na kuendelea.

Hedhi hutokea pale ambapo tishu za ukuta wa mji wa mimba zinapobomoka na kutoka kama damu ukeni.
Hata hivyo, kumekuwepo na wanawake kadhaa ambao wamekuwa wakijuta kuingia kwenye mzunguko wao kutokana na kuambatana na maumivu makali na kupelekea hata kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.

Leo ninayo orodha ya matunda ambayo yakitumika huweza kupunguza maumivu wakati wa kipindi hicho.
Matunda hayo ni haya yafuatayo:-
Nanasi.
Hili ni miongoni kati ya matunda yenye uwezo wa kupiunguza maumivu hayo yatokanayo na mzunguko (hedhi) hii ni kutokana na tunda hili kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuifanya misuli ya sehemu za siri za kike kuwa huru (kurelax) na hivyo kupunguza uwezekano wa maumivu makali.
Ndizi
Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa umuhimu wa matunda nadhani utakuwa umewahi kusikia kuhusu umuhimu wa ndizi hata kwa wanamichezo na imekuwa ikiwasaidia kurekebisha misuli na kuondoa tatizo la kukaza kwa misuli mara baada ya mazoezi, hivyo basi tunda hili pia huweza kuwasaidia wanawake ambao wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi na kupunguza au kuondoa hali hiyo kabisa.
 Pamoja na kukueleza kuwa matunda hayo huweza kupunguza maumivu wakati wa mzunguko lakini ni vyema kuzingatia kuwa matunda hayo yanapaswa kuliwa angalau siku mbili au moja kabla ya kuingia kwenye mzunguko wako ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Pia unashauriwa kunywa maji ya kutosha kipindi cha mzunguko kwani nayo huwa na nafasi kubwa ya kusaidia kupunguza kiwango cha maumivu hayo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

VIDEO:Rais wa Bolivia Anaswa Akitazama Video ya Ngono Mahakamni.

Rais wa Bolivia, Evo Morales amekumbwa na fedheha kubwa baada ya simu yae kutoa sauti zinazoaminika ni za watu wanaofanya ngono wakati akiwa katika kikao ndani ya mahakama.

Mkasa huo umetokea wakati Rais huyo akiwa katika mazungumzo na wanasheria wa kimataifa kabla ya kuchukua simu yake na muda mfupi sauti za mwanamke na miguno zinasikika kutoka kwenye simu hiyo ndipo ghafla akaitupa chini.

Video hiyo iliyovujishwa na mtandao wa LiveLeak.com  imewaacha watu wengi waliokuwa ndani ya mahakama hiyo wakicheka kufuatia tukio hilo huku baaadhi wakiishia kuguna.

Itazame hapa chini video hiyo ya mkasa wa wa Rais wa Bolivia.
 

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

HOJA Sita za rufaa ya Mbunge Lema Kusikilizwa leo.Fahamu zaidi hapa.

Hoja sita za mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kupinga kunyimwa dhamana zinatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Salma Maghimbi.

 Wakili Sheck Mfinanga anayemwakilisha Lema alisema waliwasilisha hoja hizo za rufaa kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana mteja wao.

 Lema aliyekamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma, tangu wakati huo anashikiliwa kwenye Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha ambako amekaa kwa siku 56.

 Baada ya kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Lema alipewa dhamana na Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 akidaiwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

 Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama kumpa dhamana mbunge huyo.

Mawakali wa Lema nao walikata rufaa kupinga mteja wao kunyimwa dhamana ambayo imepangwa kusikilizwa leo baada ya kukwama kwa muda mrefu kutokana na kuwapo pingamizi za kisheria zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

FARID MUSSA MAMBO SAFI, SASA KUPAA KWENDA HISPANIA LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kiungo mwenye kasi, Farid Mussa anatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda Hispania.

Mussa anakwenda kujiunga na klabu ya Derpotivo Tennerife ya Hispania.

Awali alikwama kujiunga na timu hiyo kutokana na kuwa na matatizo ya usajili.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram