Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amekitaka Chuo Kikuu cha Mount Meru kilichopo Jijini Arusha kuacha mara moja utaratibu wa kutoa alama za makisio kwa Wanafunzi wanosoma chuoni hapo na wakiendelea Serikali itakifunga chuo hicho mara moja kwa sababu utaratibu huo haujawahi kutumika katika Chuo chochote Duniani.
Waziri Ndalichako ametoa maagizo hayo alipotembelea katika Chuo hicho kuona miundo mbinu na namna wanavyo simamia utoaji wa elimu ya juu, ambapo amesema Wizara ilishatoa maelekezo kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kuwa Chuo hicho kiwaondoe Wahadhiri ambao hawana sifa za kufundisha lakini agizo hilo mpka sasa halijatekelezwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Klabu ya Manchester United imefanikiwa kurudi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) kwa kuitafuna klabu ya Chelsea goli 2-1
Chelsea walikuwa ndio wa kwanza kuliona langu la United kupitia kwa Wilian kunako dakika 32 kabla ya Romelu Lukaku kusawazisha kunako dakika ya 39 na hadi mapumziko timu zote zilikuwa 1-1.
Goli la ushindi la United limefungwa na kinda, Jesse Lingard kunako dakika ya 75 hadi filimbi ya mwisho inalia, Man United 2 Chelsea 1.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Basi la abiria (Daladala) linayofanya safari zake kati ya Mbezi na Makumbusho jijini Dar es Salaam limepinduka leo Jumatatu, Februari 26, 2018 asubuhi katika eneo la Kimara Korogwe.
Polisi wapo eneo la tukio kufanya jitihada za kuokoa watu waliokuwemo kwenye ajali hiyo ambapo basi limepinduka na kugeuka magurudumu yakawa juu.
Idadi ya majeruhi haijajulikana na iwapo kuna watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Tutakupa taarifa zaidi baadaye.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema haoni dalili yoyote ya watani wao Simba kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kwani wamepewa chuma.
Kauli hiyo ya Mzee Akilimali imekuja baada ya Simba kutinga raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa itacheza na Al Masry ya Misri Machi 6, mwaka huu.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mzee Akilimali alisema haoni dalili za Simba kufanikiwa kwenda hatua kubwa kufuatia kukutana na Waarabu ambao ni moto wa kuotea mbali katika michuano hiyo.
“Safari hii naona nao wamepata chuma kwa sababu miaka ya nyuma walikuwa wanatucheka kwamba hatuwezi kucheza na Waarabu nao ndiyo walikuwa wanajifanya wanawamudu kwa kuangalia historia.
“Lakini jambo zuri wamepata bahati na wamerejea kwenye michuano ya kimataifa ila sasa wale wanaokutana nao ni chuma cha moto, Simba hawawezi kwenda popote,” alisema Mzee Akilimali.
Al Masry ni miongoni mwa timu ambazo zinatoa upinzani mkali kwa vigogo wa soka Misri ambapo ni Zamalek na Al Ahly na sasa wapo nafasi ya nne katika Ligi ya Misri wakiwa na pointi 42.
Kocha wa Al Masry ni mshambuliaji wa zamani wa Zamalek, Hossam Hassan ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Zamalek kilichong’olewa na Simba mwaka 2003 katika Klabu Bingwa Afrika.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko kuhusu matukio ya utekaji na mauaji yanayotokea nchini, ukiitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina.
Taarifa ya umoja huo uliyotolewa leo Februari 23, 2018 inaeleza kuwa imetolewa na ushirikiano wa mabalozi wa nchi wanachama wa umoja huo wenye uwakilishi Tanzania na kuungwa mkono na mwakilishi na mabalozi wa Norway, Canada na Uswisi.
“Tunashuhudia kwa wasiwasi mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya kidemokrasia na haki za Watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, amani na uhuru.”
“Tumesikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi mwisho wa juma lililopita Akwilina Akwilini, anayeombolezwa nchi nzima. Tunakaribisha wito wa Rais John Magufuli wa uchunguzi wa haraka,” inaeleza taarifa hiyo.
Katika taarifa hiyo EU imetoa wito wa uchunguzi wa kina kwa vifo vyote vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu.
“Tunatoa pole za dhati kwa familia zao zote. Tuna wasiwasi na ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya hivi karibuni, kama vile, jaribio lililohatarisha maisha ya mbunge Tundu Lissu; kupotea kwa watu kama mwandishi wa habari Azory Gwanda na mashambulio yaliyopoteza uhai wa viongozi wa Serikali,” inaeleza EU.
Umoja huo umesema pia yametokea matukio yaliyowahusisha wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi Mkoa wa Pwani ndani ya miaka miwili iliyopita.
“Tunaungana na Watanzania katika kuwaomba wahusika wote, kutunza amani na usalama wa michakato ya kidemokrasia, watu wake na kuheshimu utawala wa sheria bila udhalimu.”
Akwilina alipigwa risasi Februari 16,2018 eneo la Kinondoni Mkwajuni, wakati Polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakielekea ofisi za msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.
Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), alipigwa risasi Septemba 7,2017 nje ya makazi yake mjini Dodoma. Kwa sasa yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu.
Azory ni mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), aliyetoweka tangu Novemba 21, 2017 Leo ametimiza siku 95 tangu alipopotea.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Unazikumbuka picha za Wema Sepetu na Diamond Platnumz zilizosambaa wakiwa wamekumbatiana kwa mahaba wakati wa sherehe ya kumkaribisha Maromboso au ‘Mbosso’ iliyofanyika mwezi uliopita katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam?
Basi tukio lile ndio limesababisha Diamond kuweza kupigwa chini na mama watoto wake, Zari The Bosslady.
Akiongea katika kipindi cha runinga cha Dira ya Dunia ya BBC Swahili, Zari amesema, “Tulikuwa tunajaribu kuona we can move from hiyo sikendo ya kupata mtoto. So we can move forward lakini vitu kama hivyo leo unasikia hivi unaona vile sijui kukumbatiana huko na maex kwenye public vitu vya kunidhalilisha, kunifanya niwe very disrespect na watoto wangu unaona tu like it’s just not right.”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
MSANII wa filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amejikuta akitafunwa na skendo ya uchawi kutoka kwa watu wake wa karibu ambao alikuwa anaishi nao, New Delhi nchini India, kutokana na mambo yake kumuendea poa huku wenzake yakibuma.
Chanzo chetu kutoka nchini humo kilidai kuwa, wasichana wengi wa Kibongo waishio India wamefurahi mno kusikia msanii huyo kafungiwa na Naibu Waziri, Juliana Shonza kufanya sanaa, sababu alikuwa anawatambia mno.
“Pretty kwa Wabongo wengi kule India wanamjua kwa kutumia ‘ndumba’ ili mambo yake yamnyookee kwani alipokuwa huko alikuwa akiwazidi wasichana wote na kila alichokifanya kilikuwa kikimnyookea tofauti na wengine.
“Hali hiyo ilisababisha minong’ono sana mpaka ameondoka na hakuna aliyempenda,” kilidai chanzo hicho ambacho kiliomba kuhifadhiwa.
Badaa ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilimsaka Pretty ambaye alifunguka kama ifuatavyo:
“Jamani mimi siyo mchawi, wananizushia sababu ya chuki zao binafsi, mimi nipo karibu na Mungu kuliko wanavyodhani, hata usiku huwa nakesha nikisali, sasa huo uchawi nafanya saa ngapi.”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amefunguka na kumtaka Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mtungi kujitafakari, kwani amedai kuwa Jaji huyo amekuwa ni mpofu kwa mambo mabaya wanayofanyiwa watu wa upinzani nchini.
Lissu amesema hayo kufuatia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuwaandikia barua CHADEMA ambayo anadai inatuhuma mbalimbali pamoja na vitisho mbalimbali
"Nimesoma barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, yenye tuhuma na vitisho vingi dhidi ya CHADEMA, bila kutoa ushahidi wowote na kwa kutegemea taarifa za upande mmoja tu, Msajili Mutungi ameituhumu CHADEMA kwa kufanya siasa za kibabe na vurugu na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Msajili Mutungi anastahili kujibiwa hadharani na kukumbushwa mambo kadhaa. Inaelekea amejisahau sana au anafikiria Watanzania ni wajinga wasioelewa mambo yake."
"Msajili wa Vyama vya Siasa amekosa sifa na uadilifu (moral authority) ya kunyooshea kidole CHADEMA au chama kingine chochote cha upinzani kuhusiana na jambo lolote linahusu Sheria ya Vyama vya Siasa na kanuni zake. Tangu 2015 nchi yetu imeshuhudia ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Vyama vya Siasa ukifanywa. Mikutano ya hadhara na maandamano ya amani, ambavyo ni haki ya vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria hiyo, imepigwa marufuku bila uhalali wowote. Msajili Mutungi hajawahi kukemea ukiukwaji huo wa sheria wala kutetea haki ya vyama vya siasa"
"Viongozi wa vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, wameuawa, wametekwa nyara na kupotezwa, wamepigwa risasi katika majaribio ya kuuawa, wameteswa, wamekamatwa na kushtakiwa kwa kesi za uongo. Msajili Mutungi amekuwa bubu na kiziwi asiyesikia wala kukemea uonevu na ukandamizaji huu dhidi ya vyama anavyovisimamia. CCM na serikali yake zimetoa hongo kurubuni madiwani, wabunge na viongozi wengine wa vyama vya upinzani kujiuzulu nafasi zao. Yote ni makosa ya maadili kwa mujibu wa sheria. Msajili Mutungi hajawahi kuliona hilo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Ratiba ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline imebadilika.
Ratiba ya awali ilieleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo baada ya kutolewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ungepelekwa nyumbani kwa dada wa marehemu eneo la Mbezi Louis na mchana kuelekea katika viwanja vya NIT, Mabibo kwa ajili ya kuagwa.
Ratiba mpya iliyotolewa leo Februari 21, 2018 na msemaji wa familia, Festo Kavishe inaeleza kuwa baada ya mwili kutolewa MNH, utapelekwa NIT kwa ajili ya kuagaw.
Kavishe ameiambia MCL Digital kuwa ndugu wataanza safari kuelekea NIT saa 5:00 asubuhi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejikuta matatani baada ya wadau, maofisa wa benki na viongozi wa dini kuhoji uhalali wa mamlaka hiyo kuweka hadharani taarifa za fedha za Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF).
Juzi, TRA ilitoa taarifa ya uchunguzi ilioufanya kuhusu kauli ya kiongozi wa kanisa hilo Askofu Zachary Kakobe aliyoitoa wakati wa ibada ya mkesha wa Krismasi mwishoni mwa mwaka jana kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali.
Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alisema wangefanya uchunguzi kuhusu kauli hiyo, lakini taarifa aliyoitoa juzi ilionyesha kuwa Askofu Kakobe hana akaunti katika benki yoyote nchini bali ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti ya kanisa analoliongoza.
Kichere alisema akaunti za kanisa hilo zipo katika benki ya NBC zikiwa na zaidi ya Sh8 bilioni na zinatokana na fedha za sadaka, zaka na changizo zinazotolewa na waumini.
Kichere alipotafutwa na Mwananchi jana kuhusu hatua ya kutangaza taarifa za kifedha za kanisa hilo alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari inaeleweka na inajieleza hivyo hawezi kutoa maoni zaidi.
“Wakati nataka kufanya uchunguzi nilieleza wazi nia yangu, hata baada ya kumaliza uchunguzi niliona ni busara kusema yaliyobainishwa katika uchunguzi, sitaki ‘ku-comment’ (kutoa maoni) zaidi, mjadala wa masuala ya Kakobe ulishafungwa,” alisema Kichere.
Akizungumzia taarifa ya TRA, ofisa mwandamizi wa benki moja nchini ambaye hakutaka utambulisho wake uwekwe hadharani alisema kitendo cha mamlaka hiyo kutoa taarifa za fedha kwa umma ni uvunjifu wa sheria.
Alisema kwa mujibu wa sheria taarifa za kibenki zinapokuwa zinahitajika na vyombo au mamlaka za Serikali zinaweza zikatolewa mahakamani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa au polisi lakini si kwa umma.
Alisema Askofu Kakobe ana nafasi kubwa ya kuwafungulia mashtaka uongozi wa benki na mamlaka iliyotoa taarifa zake kwa umma.
Mkurugenzi mtendaji wa benki (jina limehifadhiwa) alipoulizwa kuhusu utaratibu wa kawaida wa utunzaji wa siri za mteja alisema sheria ya huduma za benki inaelekeza vizuri kuhusu jambo hilo lakini taarifa zinaweza kutolewa kwa mujibu wa sheria kutokana na mazingira na madhumuni fulani.
Alisema hata pale ambapo taarifa zinaonekana ni muhimu kutolewa kwa mamlaka yoyote ya Serikali iliyokidhi vigezo, bado hairuhusiwi kuziweka kwa wazi bali inapaswa kuzitumia kwa kazi yake tu kwa kuwa kuzichapisha kwa namna yoyote ni kuvunja sheria.
“Suala la taarifa za mteja ni siri kubwa ndiyo maana hata ofisa wa benki hana namba ya siri ya mteja. Inapotokea taarifa za mteja zimetolewa halafu zikachapishwa na ile mamlaka iliyopewa taarifa hizo, mteja anaweza akafungua kesi ambayo ni kubwa dhidi ya benki na hiyo mamlaka,” alisema.
Suala hilo halikuwapita viongozi wa dini, kwani nao walikuwa na maoni yao.
Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe alisema hatua hiyo ni mbaya na haikubaliki kwa taasisi za dini.
“Hiyo ni mbaya sana. Kama Askofu Kakobe asingesema kile alichosema asingechunguzwa. Kwa hiyo kama hutaki kuchunguzwa usiseme kitu? Kwa hiyo maisha yetu yanakwenda mbali hadi kwenye mali za kanisa?” alihoji Askofu Bagonza.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Alinikisa Cheyo aliyeitaka TRA kufuata maadili ya kazi.
“Nafikiri TRA wana maadili wanaposhughulika na wateja wao. Huwezi kuweka wazi madeni na mali za mteja wako. Si makanisa tu hata wateja wa kawaida, labda ni kwa sababu ya mlolongo wa yaliyotokea.” alisema Dk Cheyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
VILIO na simanzi vimetawala wakati wa kuchukua mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini aliyeuawa kwa kupigwa risasi Feb 16, 2018.
Mwili wa Akwilina umechukuliwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa NIT k wa ajili ya kuagwa kabla ya kupelekwa nyumbani kwao Rombo kwa mazishi.
Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi huo liko katika gari maalumu la kubebea maiti.
Baada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, saa 10 jioni safari kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi itaanza. Akwilina atazikwa kesho. Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amewasili nchini leo alfajiri Feb. 22, 2018 kwa ajili ya mkutano wa FIFA unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais huyo wa FIFA akiwa uwanjani hapo baada ya kuwasili alipata fursa ya kuzungumza na waziri Mwakyembe ambapo alimtaja nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, anayecheza soka la kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji.
“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania, Mbwana Samatt, anayecheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za shirikisho siku za nyuma, lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF na FIFA,” alisema Infantino.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa muigizaji Irene Uwoya ameamua kuyaanika ya moyoni kuhusu wanawake ambao hawatoi ushirikiano kwa wanawake wenzao na hupenda kuona wenzao wakianguka au kufeli kimaisha ambapo hufurahishwa na jambo hilo.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Irene Uwoya ameandika
“Hivi kwanin wanawake tunakuwa hatupendani???yani najiulizaga sana badala sisi tushirikiane ndo kwanza tunarudishana nyuma…mtu akifanya kitu kizuri au biashara ndo wa kwanza kuponda na kurudishana nyuma…yani unamskia mtu kabisa anakuponda mbayaaa afu hujawah ata kugombana na nae na pengine unamsaidiaga tu sana”
“Yani unashangaaa wanaokuunga mkono ni wanaume badala ya wanawake wenzako afu ukifanya mabaya ndo anakusifia balaaah ili uwendeleee kuharibuuu…!afu Sasa yeye akifanya lake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwah kufanya hivyo!!!yani kuna mijitu ina rohooo daaahhh!!!”
Mimi Sasa hiv nimeamua si support mtu yeyote asie ni support na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiye kuwa na humuimu kwenye maisha yako haina haja ya kuwa sehemu ya maisha yako atakurudisha nyuma tu!!!”
“Achana na watu wasio na faida wala mchango wowote kwenye maisha yako badilika!!!achana na marafiki wanao kushauri stareheee tu sikuzote…kaaa fikiri katika hao rafiki zako kuna siku atamoja walikushauri kitu cha maana cha kuingiza pesa??? au bataaa tuuu??? punguza watu wasio na mashiko kwenye maisha yako punguza marafiki wasio na faida” -Uwoya Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah, ameushangaza umma baada ya kumpongeza mume wake kwa kuongeza mke wa pili, kwani ni kitendo cha nadra sana kwa wanawake kufanya hivyo licha ya kuwa misingi ya dini inaruhusu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkuu wa wilaya huyo ameandika ujumbe huku akiujulisha umma kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.
“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi”, ameandika Bi. Zainab Abdallah.
Mheshimiwa huyo wa serikali ya wamu ya tano aliendelea kuandika kuwa ...”Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Asasi za Kiraia nchini zimetaka iundwe Tume huru ya uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwiline itakayoundwa na Taasisi za Dini, Vyombo vya Habari, Majaji, Mahakimu, Polisi na Baraza la Vyama vya Siasa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Equality for Growth, Jane Magigita amesema kuwa Asasi za kiraia zimesikitishwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Tunapendekeza iundwe Tume huru ya uchunguzi itakayohusisha Azaki, Taasisi za dini, vyombo vya Habari, Baraza la vyama vya siasa, wanahabari, Majaji, Polisi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kufanya uchunguzi juu ya vifo na vitendo vya utekwaji na utesaji,”-Magigita
“Pia ni kosa kubwa kuwaachia Polisi kujichunguza wenyewe katika matukio yanayowahusu,” -Magigita
Mbali na hilo, pia ameiomba Serikali itazame upya suala la upatikanaji wa Katiba mpya na mchakato wake uanze mwaka huu kwani ndiyo suluhisho la matatizo mbalimbali yanayotokea katika Jamii kwa sasa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
SIMBA imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya jana kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendarmarie nchini Djibouti.
Mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, aliifungia Simba bao hilo pekee katika dakika ya 53 na kuifanya Simba sasa kukutana na 'Waarabu' wa Al Masry.
Simba imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 kufuatia ushindi wa bao 4-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Al Masry yenyewe pia imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya jana kubanwa na Green Buffaloes na kutoka sare ya bao 1-1 nchini Zambia.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Misri, wenyeji walishinda kwa mabao 4-0.
Simba sasa itakuwa na kibarua mbele ya Waarabu hao, katika kuwania kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.Timu hizo zitakutana kati ya Machi 6, 7 mwaka huu, huku Simba wakianzia nyumbani kabla ya kuwafuata Al Masry wiki mbili baadaye.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameondoka nchini leo kuelekea Uganda kushiriki Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala.
Rais Magufuli ameagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF ), Jenerali Venance Mabeyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa