Monday, 26 March 2018

Irene Amvaa Wema Sepetu Amtupia Dongo Zito Kisa ni Diamond.

Video vixen aliye jizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii Rayvanny Irene, amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Wema Sepetu huku ikidaiwa kisa ni penzi la Diamond.

Tangu Zari aweke wazi kuwa kaachana na Diamond na kuwa single Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwenye social media juu ya nani hasa anayechukua nafasi ya Zari na moja kati ya Wanawake waliotajwa kuwa na uhusiano na Diamond kwa sasa ni Irene na Wema.

Kuna stori ili trend sana kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo ambapo ilisemekana kuwa Irene na Wema wamepeana kichapo cha maana baada ya kugongana Madale nyumbani kwa Diamond.

Stori hiyo ilidai kuwa Diamond anatoka na Irene na Wema kwa wakati mmoja na wikiendi hii Irene kamtupia dongo Wema ambapo amemcheka kuwa anajiita African beauty wakati hata kiwanja hana!.

African beauty ni wimbo mpya wa Diamond na siku wimbo huo ulipotoka wasanii mbali mbali wa WCB akiwemo Harmonize alimtunuku Wema jina la African beauty jambo ambalo lilimfanya Wema ajitambe kuwa ni African beauty.

Fununu za Irene kuwa na Mahusiano na Diamond zilianza siku nyingi sana wakati bado Diamond yuko na Zari ingawa Diamond alikuwa anakataa kuwa hana Mahusiano naye.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Saturday, 24 March 2018

Diamond amtaka Lulu Diva kumzalia mtoto Rich Mavoko.

Baada ya kukanusha kwa muda mrefu, hatimaye imebainika kuwa Rich Mavoko na Lulu Diva ni wapenzi.

Aliyeweka wazi hilo ni Diamond Platnumz ambaye anafanya kazi na Rich Mavoko kupitia label yake ya WCB. Katika kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Lulu Diva, Diamond amemwandika haya mrembo huyo.

We @luludivatz nae Utulete Mtoto sasa, Tushachoka picha zenu za Kuviziwa kwenye ma Parties😏👌🏼#AfricanBeauty

Utakumbuka Fiesta ya Dar es Salaam iliyofanyika November, 2017 kuna picha zilisambaa mtaandaoni zikiwaonyesha Rich Mavoko na Lulu Diva katika mapozi ya kimahaba ingawa wenyewe walikanusha na hilo pia ila kwa kauli hii ya Diamond ni wazi lilokuwa likisema lipo. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Okwi,Bocco Waahidi Kupata Ubingwa wa Ligi Kuu.

BAADA ya Simba kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika, mastraika wa timu hiyo John Bocco na Emmanuel Okwi kwa pamoja wameapa kufia uwanjani ili Wekundu wa Msimbazi wabebe ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba iliondolewa na Al Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam halafu ugenini wakatoka suluhu.

Kutokana na hali hiyo, Okwi na Bocco wamesema lengo lao sasa ni kuhakikisha wanapambana kufa na kupona kwenye Ligi Kuu Bara ili waweze kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa.

Simba inaongoza katika ligi kuu ikiwa na pointi 46 sawa na Yanga, inayoshika nafasi ya pili, lakini wenyewe wana tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi alisema, mipango yao ya kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho imekwama, sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye ligi kuu.

“Tunarudi kujipanga kwenye ligi kuu, kwani ndiyo sehemu pekee tunapotakiwa tupambane kufa na kupona ili mwakani tuweze kushiriki tena michuano ya kimataifa, tutapambana tuwe mabingwa,” alisema Okwi.

Kwa upande wake, Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba, yeye alisema; “Kiu yangu na wachezaji wenzangu ni kuhakikisha tunatwaa taji la Ligi Kuu Bara, maana ndiyo silaha pekee tuliyonayo kwa sasa, hiyo ndiyo tiketi ya sisi kucheza mechi za CAF mwakani.

“Pia tunajua furaha ya mashabiki wa Simba kwa sasa ni kuona tunatwaa ubingwa na siyo kitu kingine, hivyo tumejipanga kuhakikisha hilo linatokea bila tatizo.”

Simba leo Jumamosi inatarajiwa kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Njombe Mji, Aprili 3, mwaka huu. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 21 March 2018

Mahakama Kuu Iimetoa Amri kwa Serikali Kupeleka Majibu Juu ya Abdul Nondo.

Mahakama Kuu leo imetoa amri kwa serikali kuweza kupeleka majibu ya maombi yaliyofunguliwa na Mawakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Abdul Nondo kujibu kesi ya kutompeleka Mahakamani kwa zaidi ya siku 10 tangu kukamatwa kwake.


Amri hiyo imetolewa leo Jumatano ya Machi 21 ambapo Mahakama kuu mbele ya Jaji Sameji  iliwataka DCI,IGP na AG kufika mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtka juu ya Nondo ambapo leo majibu ya maombi hayo wyametakiwa yapelekwe Machi  26 na walalamikaji  kupeleka majibu yao ya nyongeza yapelekwe Machi 27.

Aidha  mahakama inatarajiwa kusikiliza maombi ya pande zote mbili 04/08/18 kutoa hatma ya Abdu Nondo.

Kwa upande mwengine kesi ya mwanafunzi huyo (Nondo)  iliyosikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 26 March 2018 ambapo Hakimu atatoa uamuzi kwamba mshitakiwa apewe dhamana ama asipewe dhamana, mshitakiwa amerudishwa rumande.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Khadija Khopa Achoka Kuwa Single Ataka Mwanaume wa Kumuoa "Nataka Mume Sipendi Dhambi".

Malkia wa Mipasho nchini Tanzania asiyekuwa na mshindani, Khadija Kopa ametangaza rasmi kuhitaji mume wa kumuoa ili aweze kuishi naye huku akiweka vigezo vyake kuwa hataki aliyechini ya miaka 40 kwa madai hawezi kufundisha tution.


Khadija Kopa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.

"Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume aliyekuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua ninataka nini, atakayeweza kuijali familia yangu pamoja na watoto wangu, awe mnene kidogo na sio mwembamba, awe na rangi yeyote na kabila lolote lile kwasababu mimi sina ubaguzi katika vitu hivyo", amesema Khadija Kopa.

Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema "napenda mwanaume mfanyakazi maana kupata pesa ni majaliwa ila asiwe mwanaume wa kulala nyumbani akanitegemea mimi nikafanye kazi ili yeye aje kula maana maisha ni kusaidia nasio kuegemea upande mmoja tena wa mwanamke".

Aidha, Khadija Kopa amesema sababu kubwa iliyompelekea mpaka sasa kutoolewa ndoa nyingine baada ya aliyekuwa mume wake kufariki ni kutokana na kuwa na wasiwasi na wanaume wa sasa.

"Nina wasiwasi kwa mwanaume atakayekuja kunioa kwa sasa, maana najiuliza mengi je atakuwa na huba kama marehemu mume wangu ndio maana mpaka sasa sijaolewa kwa kuwa nafikiria sana. Mume wangu aliyefariki alikuwa ni mwenye huba, mwenye kunijali, nimekaa naye miaka yote sijawahi kugombana naye, nilikuwa natamani kumuona akinuna ananuna vipi, alikuwa na vigezo vyote", amesisitiza Khadija Kopa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Necta Yafanya Mabadiliko Mtihani Darasa la Saba.

Wanafunzi wa darasa la saba ambao watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa utungaji  wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi .

Mabadiliko hayo yamefanywa na Baraza la Mitihani la Taifa  (Necta) jana na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.

Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.

Nchimbi amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk).

Amesema maswali 40 kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.

Kutokana na muundo huo mpya, Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mwakyembe Amshukia Diamond, Asema Umarufu Utamkosti, Awezi Bishana na Shonza na Atapotea Kubishana na Serikali.

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi nibmaarufu kiasi gani."

"Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo." 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 20 March 2018

Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata Ajali Kigoma.

Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kwwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika .
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Monday, 19 March 2018

Zitto Kabwe Alishitaki Jeshi La Polisi Mahakamani.

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo, Kabwe Ruyagwa Zitto amefunguka na kusema kuwa chama chake tayari kimefungua kesi ya Kikatiba katika mahakama Kuu Dar es Salaam kulishtaki jeshi la polisi.

Zitto Kabwe amesema hayo leo Machi 13, 2018 wakati akitoa tathmini ya ziara alizofanya kutembelea Madiwani katika kata mbalimbali nchini zinazoongozwa na ACT Wazalendo ambapo amedai katika ziara hiyo wamebaini mambo mengi ikiwa pamoja na hali ya maisha kuwa ngumu sana, migogoro ya ardhi, kukosekana kwa huduma ya Maji safi na salama, ukosefu wa huduma bora za afya, tatizo la Miundombinu ya Usafirishaji.

Kiongozi huyo aliendelea kuweka wazi mambo mbalimbali ambayo wamefanikiwa kuyaona katika ziara hizo kuwa ni pamoja na  ukosefu wa pembejeo za Kilimo, ukosefu wa masoko ya mazao ya wavuvi, wakulima na wafugaji, kushuka kwa bei ya mazao yao, kupanda kwa gharama za maisha ya watu, kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi, upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, vyoo pamoja na walimu, na kuzorota kwa hali ya usalama wa wananchi pamoja na mali zao, hali mbaya ya ajira kwa vijana pamoja na uminywaji mkubwa wa demokrasia na uhuru wa watu kukusanyika na kujieleza.

"Tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli, ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza. Tunaamini Mahakama itatenda haki kwenye suala hili" alisema kiongozi huyo

Aidha Zitto Kabwe ametoa ushauri kwa serikali kuhusu suala la Demokrasia nchini na kusema kuwa mazungumzo ya kitaifa ndiyo yanaweza kuwa na jibu kuhusu masuala haya na kuleta utatuzi juu ya jambo hili.

"Demokrasia na Ustawi wa Taifa tunaendelea kusisitiza rai yetu kuhusu umuhimu wa kuitisha Mkutano wa Kitaifa wa maridhiano ya kisiasa kama jukwaa la kuzijadili changamoto za uendeshaji wa siasa nchini. Jambo hilo litaondoa uadui unaoendelea kukua sasa kati ya serikali na wananchi, viongozi wa dini, mashiriki yasiyo ya Kiserikali, taasisi za wanafunzi, pamoja na vyama vya Upinzani. Tunaamini mazungumzo ya Kitaifa ndio jambo sahihi la utatuzi wa suala hili" alisisitiza Zitto Kabwe

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday, 16 March 2018

Baada ya Magari ya Mwendokasi Kusitisha Huduma ya Usafiri Daladala, Bodaboda Zatumia Njia ya Mwendokasi.

Baada ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dart) kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, baadhi ya magari madogo, daladala na bodaboda wametumia fursa hiyo kupitisha magari yao katika barabara zinazotumika na magari hayo.

Mwananchi limeshuhudia daladala zikipita katika vituo hivyo huku zikishusha na kupakiza abiria katika kila kituo cha mwendokasi, huku trafiki wakielekeza baadhi ya magari kutoka kwenye barabara hizo.

Hata hivyo vituo vingi vya mwendokasi vimefungwa isipokuwa kituo cha Ubungo ambacho wahudumu wameonekana wamelala huku kukiwa hakuna abiria  wanaoingia katika kituo hicho.

Dereva wa daladala linalofanya safari zake Mbagala Rangitatu - Simu 2000 Jafari Himid amesema kutokana na foleni iliyopo katika barabara hiyo, wameamua kutumia barabara za mwendokasi ili kuokoa muda.

"Bila kufanya hivi hatuwezi kuwahisha abiria na hizi barabara leo hazina matumizi, hata trafiki wanatuachia hawajatukamata," amesema Jafari.

Hata hivyo barabara ya Morogoro Road ina foleni kubwa inayosababishwa na kipande cha barabara ya jangwani kujaa tope. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 15 March 2018

Download wimbo mpya wa Rockygazim unaoitwa "Nipokee".

https://my.notjustok.com/track/download/id/313584


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Video: Uzinduzi wa Diamond Watikisa Kenya Awaliza Wakenya Jukwaani na Historia ya Maisha Yake.

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezindua rasmi albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’ jijini Nairobi na kufanya bonge la shoo akiwa na timu nzima ya WCB.

Mbali na WCB, wasanii wengine waliopada jukwaani na kutikisa katika shoo hiyo, ni msanii wa Marekani, Omario.


Albamu mpya ya Diamond imesheheni ngoma 20 kali zikiwemo alizowahi kuzitoa kipindi cha nyuma na nyingine mpya.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: TFF Yamfungia Maisha Kujihusisha na Msuala ya Soka Michael Wambura.

Habari za ndani zinasema Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura kutojihusisha na soka maisha yake yote.


TFF imetangaza rasmi maamuzi ya Kamati hiyo saa 6 mchana muda ambao Wambura pia amepanga kuzungumza na waandishi wa habari baada katika hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.


Sekretariati ya Shirikisho la soka Tanzania TFF ilimfikisha Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kwenye kamati ya maadili akikabiliwa na tuhuma tatu ikiwemo kupokea fedha za malipo TFF za malipo ambayo hayakuwa halali.

Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TFF, baada ya kamati ya maadili kupokea malalamiko yanayomhusu Wambura na kukutana jana (Machi 14, 0218) kwa ajili ya kujadili, imemfungia maisha Wambura kujihusisha na masuala ya soka.

Kwa mujibu wa afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo, Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo, kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi. Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea


Emmanuel Muga amesema hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14, 2018).

“Ni kweli sikupewa nafasi ya kumtetea kwa sababu kamati ilikuja ikiwa na dhamira yake kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo. Kwa hiyo nilivyowasilisha masuala ya kisheria ambayo ni ya kikanuni, kamati ilikataa ikasema sisi tunaamua tunavyoona”-Emanuel Muga, Wakili wa Wambura.

“Kwa hiyo wakalifunga suala kwamba yanaenda kufanywa maamuzi, lakini hayo maamuzi yatafanyika wakati Wambura hajasikilizwa na Wakili wake hajasikilizwa.” 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nicki Minaj – Diamond.

Zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nicki Minaj – Diamond
Msanii Diamond Platnumz bado anaonekana kutokubaliana na uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) wa kuzifungia nyimbo zake mbili ambazo ni Waka na Hallelujah.

Muimbaji huyo akizungumza na Classic FM nchini Kenya amesema serikali ni lazima iangalie maudhui ya wimbo husika na msanii husika nini hasa alilenga.

“Huwezi kuimba nyimbo za mapenzi usitaje maneno ya kimahaba, ni uongo kwa sababu utakuwa haufikishi ujumbe,” amesema.
“Nyimbo kama Waka na Hallelujah ni nyimbo ambazo nilifikiria kufanya kitu ili soko lingine watusikilize, serikali lazima ielewe. Na kinachouma zaidi zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nick Minaj, so ni lazima tuangalie,” amesisitiza Diamond.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 14 March 2018

BREAKING: Goodnews Kwa Watanzania Watakaopenda Kufanya kazi Mradi wa Bomba la Mafuta.

Watanzania watakaopenda kufanya kazi katika Bomba la Mafuta, Bonyeza PLAY hapa chini kutazama. VIDEO: 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Irene Uwoya Ampa Onyo Kali Dogo Janja " Thubutu Uwone Tena Ndo Utanijua ".

Mke wa msanii wa muziki Dogo Janja, Irene Uwoya ametoa majibu juu ya habari zilizopo za mumuwe kutaka kuongeza mke wa pili hadi wanne.

Uwoya ametoa majibu hayo baada ya kukuta habari zimezagaa katika mitandao mbalimbali juu ya mpingo ya mumuwe aliyoweka ya kutaka kufikisha idadi ya wake wanne katika ndoa.

“Ndoutajua mim Kabila gani…thubutu uwone tena wasikudanganye @dogojanjatz,” ameandika mrembo huyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram mapema leo baada ya kuona stori za mumuewe za kumuongezea mke zikitawala.

Katika kipindi cha The Playlist ya Times Fm kilichoruka juzi ( 12-03-2018) mkali huyo wa ‘Wayu Wayu’ alidai kuwa anampango wa kuongeza mke wa pili hadi wanne kila baada ya miaka 10. 
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 6 March 2018

Kumbe Daxx Ndo Baba Kijacho wa Dayna Nyange..... Dayna Afunguka A-Z "Ujauzito Haujifichi".

Msanii Dayna Nyange amezungumza na kuelezea skendo zilizopo za yeye kuhusishwa kutoka na Daxx ambaye ni Fashion Model na ameonekana kwenye video mpya ya Dayna Nyange ya ‘Sale Sale’ ikiwa ni pamoja na kuhusishwa kuwa mjamzito.

Dayna Nyange amesema kwamba yeye anamahusiano na Daxx lakini siyo ya kimapenzi kwani yeye anaye mpenzi wake na ishu ya yeye kuwa na mimba kasema hajawahi kusema kama ni mjamzito lakini Mimba haijifichi na kama ipo watu wataona na waandae Pampas na maziwa ya mtoto.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Gazeti Lililomuandika Mange Vibaya Lapewa Onyo Kali na Serikali.

Serikali imelionya Gazeti la Tanzanite kwa kuchapisha picha za utupu kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada msemaji wa serikali Dkt. Hassan Abbas kuahidi kulichukulia hatua gazeti hilo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na ukakasi wa habari zake pamoja na picha wanazochapisha.


Onyo hilo limetolewa hii leo mjini Dodoma na Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wametoa onyo kwa Gazeti hilo kwakua ni jipya pia ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo hivyo ni bora kujirekebisha.

Amesema kuwa Gazeti hilo halikuwa na kosa katika maudhui ya kuandika ila kosa kubwa ni kutumia picha za utupu, hivyo kwenda kinyume na maadili.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: Moto Mkubwa Waunguza Soko Mbagala.

Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii Machi 6, 2018.

Sehemu iliyoathirika zaidi ni ile ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika  kuzima moto huo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Picha: Hivi Ndivyo Polepole Alivyonusurika Kufa Baada ya Msafara Wake Kupata Ajali.

Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la kijiji cha Nyamidaho, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota V8 yenye namba T150 EWE iliyokuwa ikiendehswa dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hosiptali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Poplepole amewasili leo mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa