Monday, 3 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Mulumbu mchezaji wa Norwich City kuukosa mwanzo wa msimu England.




Kiungo mpya wa timu ya Norwich City Youssouf Mulumbu ataukosa mwanzo wa msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Kiungo huyu aliyejiunga na Norwich katika majira ya kiangazi amevunjika mfupa wa kidole gumba cha mguuu hivyo atakua nje kwa wiki kadhaa kwa ajili ya matibabu
Mulumbu ambae ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliumia katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi utakaoanza jumamosi ijayo.
Kocha wa Norwich Alex Neil amesema itamchukua wiki kadhaa kwa mchezji huyo kupona na kuweza kuwa fiti kwa mikikimikiki ya ligi kuu ya England.
Chazo
             BBC.

#Breaking news>>>Kundi la waislamu lahukumiwa jela miaka 22.




Mahakama moja nchini Ethioipia imeliukumu jela miaka 22 kundi moja la waislamu chini ya sheria tata ya kukabiliana na ugaidi.
Washukiwa hao 18 walishtakiwa mwezi uliopita kwa mashtaka ikiwemo lile la ugaidi na njama ya kubuni taifa la kiislamu.
Walikamatwa miaka mitatu wakati wa maandamano ya kupinga serikali kuingilia maswala ya kidini.
Walikana mashtaka hayo na kulalama kwamba walinyanyaswa wakati walipokuwa kizuizini.
Wakati wa ziara ya rais Obama nchini humo baadhi ya wanaharakati walimueleza kuhusu kesi hiyo.
Chanzo
               BBC.

#YALIYOJIRI>>>Mwigulunchemba Mbunge wa Iramba-CCM Ashinda Kura za Maoni.




Mbunge wa Iramba-CCM na alikuwa gombea alieshindwa kupita kwanye kura za kugombea Uraisi ndani ya CCM leo hii kashinda kura za maoni ya kugombea Ubunge huko Iramba Kwa Asilimia 99 %.

#YALIYOJIRI>>>Mtikila aandaa makabrasha ya kumburuza Lowassa,Magufuli Kortini.




MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amesema chama chake kinaandaa taratibu za kwenda

mahakamani ili kumshtaki mgombea urais mteule wa CCM, Dkt. John Magufuli na mgombea urais wa CHADEMA, Bw. Edward Lowassa.

Alisema wagombea hao kwa nyakati tofauti, wameshiriki kuiingizia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha ambapo wanasheria wa chama hicho wapo katika hatua za mwisho ili wafunguliwe mashtaka mahakamani.

Mchungaji Mtikila aliyasema hayo Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa, wagombea hao wamepoteza sifa za kuwania nafasi hiyo akidai hawana vigezo kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza kuwa, Bw. Lowassa, anahusishwa na sakata la kampuni ya kufua umeme ya Richmond na kuishangaa CHADEMA akidai chama hicho kilipata umaarufu wa kupinga vitendo vya ufisadi lakini wamempokea Bw. Lowassa na ana tuhuma kama hiyo.

"Kipindi cha nyuma, CHADEMA walianzisha operesheni nyingi ikiwemo ya Sangara na Movement for Change zikiwa na lengo la kupinga ufisadi, kwanini wamempokea Lowassa waliyemuita fisadi.
"Hii ina maana kuwa, ndani ya CHADEMA hakuna siasa, nawapongeza baadhi ya viongozi wa chama hicho na wanachama wao ambao kimsingi hawakubaliani na matakwa ya viongozi wa juu," 
Akimzungumzia Dkt. Magufuli, alimhusisha na tuhuma ya uuzwaji wa nyumba za Serikali akidai kitendo hicho kimeisababishia hasara Serikali lakini hakupelekwa mahakamani kwa kutumia madaraka yake vibaya kama ilivyokuwa kwa Basil Mramba, Daniel Yona ambao hivi sasa wanatumikia kifungo gerezani.

Alisema nyumba hizo zilikuwa makazi ya viongozi kama Majaji, Makatibu Wakuu na Watendaji waandamizi serikalini ambao wengi wao walilazimika kuishi hotelini kwa gharama za Serikali.
Chanzo
                 MAJIRA.

#YALIYOJIRI>>>>Kutoka IKULU Rais kikwete akiwaaga mamia ya wakazi wa Tanga waliojitokeza katika mkutano mkubwa wa hadhara leo.



Raisi Jakaya Kikwete akiwaaga wakazi wa tanga hii leo.

#YALIYOJIRI>>>Msanii Msagasumu ambae anaimba nyimbo za Vigodolo awagumzo EATV kwenye kipindi cha Mkasi.

Msanii wa nyimbo za Vigidolo awagumzo baada ya kuzungumzia manene ya kiuni ambayo mashabiki wake wanayapenda sana kingine ni kumuona Salama siku ya kwanza,Ata ivyo uyo msanii aliimba wimbo wa Timu ya Simba na Yanga nyimbo zake zimesikika sana kwa waendesha boda boda na kwenye part za uswailini ambazo zina kesha kwa mahalufu Kigodolo.

#YALIYOJIRI>>>> vigogo wa ccm wajiunga na Chadema katika kikao katika ukumbi wa Kisange Conference Center jijini Dar es salaam leo.


Matson Chizii, Ole Medeye, Mgana Msindai vigogo wa ccm waliojiunga Chadema katika kikao katika ukumbi wa Kisange Conference Center jijini Dar es salaam leo.

EdwardLowassa akiongea na wajumbe katika Kikao cha Baraza Kuu katika ukumbi wa Kisange Conference Center leo