Monday 3 August 2015

#Breaking news>>>Kundi la waislamu lahukumiwa jela miaka 22.




Mahakama moja nchini Ethioipia imeliukumu jela miaka 22 kundi moja la waislamu chini ya sheria tata ya kukabiliana na ugaidi.
Washukiwa hao 18 walishtakiwa mwezi uliopita kwa mashtaka ikiwemo lile la ugaidi na njama ya kubuni taifa la kiislamu.
Walikamatwa miaka mitatu wakati wa maandamano ya kupinga serikali kuingilia maswala ya kidini.
Walikana mashtaka hayo na kulalama kwamba walinyanyaswa wakati walipokuwa kizuizini.
Wakati wa ziara ya rais Obama nchini humo baadhi ya wanaharakati walimueleza kuhusu kesi hiyo.
Chanzo
               BBC.

0 comments:

Post a Comment