Baada
ya kufanikiwa kupata timu nchini Oman na kuachana na Azam FC, taarifa
zinaeleza, mshambuliaji Kipre Tchetche ametoweka nchini humo.
Taarifa zinaeleza kuwa, Kipre ameondoka nchini Oman wakati ligi ikiendelea na kuiacha timu ya Al Nahdha kwenye mataa.
Mmoja
wa marafiki wa karibu aliye nchini Oman, amesema viongozi wa klabu hiyo
walikuwa wakilalamika kuhusiana na raia huyo wa Ivory Coast.
“Ameondoka
na wanalalamika sana, sijui ni kwa nini. Wanalalamika kwa kuwa hawajui
sababu na taarifa zinasema yuko kwao Ivory Coast,” alisema.
Juhudi
za kumpata nchini Ivory Coast kupitia simu ya mkononi, zilikuwa mtihani
ingawa uthibitisho ulipatikana kwamba ana mpango wa kuondoka zake
kwenda kucheza Ulaya.
“Kweli
yupo hapa Abidjan. Kipre ana mpango wa kwenda Ulaya, ingawa hatujajua
ni nchi gani,” alisema rafiki yake wa karibu ambaye alianika awali
uamuzi wake wa kucheza Oman.
“Amepata
timu na kule Oman hakufurahia hali ilivyo na mazingira. Sasa
anashughulikia visa, halafu atakwenda Ulaya. Nitawaambia,” alisema
rafiki huyo.
Kipre
aliondoka nchini wakati wa mapumziko lakini hakurejea Azam FC, taarifa
zilizoelezwa kutoelewa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.
Baada
ya kuwa na taarifa huenda angetua Yanga, baadaye alisaini Al Nahdha ya
Oman ambayo huvaa jezi ya kijani na nyeupe. Lakini mwisho, sasa amerejea
Ivory Coast.
Juhudi
za kuendelea kumtafuta Kipre ili atoe ufafanuzi kuhusiana na hili
kwamba anakwenda Ulaya, au anataka kurejea Tanzania na itakuwa timu
gani, zinaendelea.
<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>
<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>
0 comments:
Post a Comment