Home »
Burudani
» #BURUDANI>>>>>>Chidi alikuwa apelekwe Ulaya kwenye matibabu kama angemaliza muda wa matibabu Sober House – Kalapina.Fahamu zaidi hapa.
Rapper Kalapina mmoja kati ya wadau ambao walimsaidia Chidi Benz
kumpeleka Sober House amefunguka kwa kusema kuwa kitendo cha Chidi Benz
kukatisha muda wa matibabu akiwa Sober House kumemkosesha vitu vingi
pamoja na kupelekwa Ulaya kwa ajili ya matibabu.
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumanne hii,
Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka
‘sober house’.
“Chid Benz hakumaliza muda wa matibabu alivyotoka ‘sober house’ ndani ya
siku 28, kwahiyo mi namuomba afikirie faida alizozipata sober na faida
anazozipata sasa hivi akiwa mtaani, nafasi bado ipo kwake kwa sababu
tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa, kwa hiyo anatakiwa
atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza kujisahihisha”,
alisema Kalapina.
Kalapina amesema Chidi Benz alipata wafadhili wa kumpeleka nchi za nje
kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kitendo hicho.
“Kulikuwa kuna safari ya yeye na Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili
walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa matibabu zaidi, lakini ilitakiwa
subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka kukaa sober anataka kukaa
mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena ku’invest hela yao
inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina
Related Posts:
Hatma ya Chege na Temba Sasa Hadharani..!!!.Fahamu zaidi hapa.
Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Chege Chigunda amesema yuko mbioni
kukata kiu ya mashabiki wa 'Chege na Temba' kwani bada ya kutoa ngoma
yake ya Kelele za Chura, ngoma inayofuata ni yake na swahiba wake Mh.
Temba kuto… Read More
Kauli ya Vanessa Mdee Baada ya Kutajwa na RC Makonda Kwenye Listi ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya.Fahamu zaidi hapa.
Iliwashangaza
wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya
madawa ya kulevya.
Ni shutuma nzito, na hata kabla uthi… Read More
Nape aingilia kati sakata la wasanii wa ‘unga’..Aongea Mazito ..Msikilize hapa.Fahamju zaidi hapa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia
kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika
na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda
… Read More
DIAMOND AMWAALIKA RC MAKONDA NA WEMA SEPETU KWENYE 40 YA MTOTO WAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
DIAMOND AMWAALIKA RC MAKONDA NA WEMA SEPETU KWENYE 40 YA MTOTO WAKE
WALIOTAJWA HAPO WANAOMBWA KUFIKA NYUMBANI KWA BWANA NASIBU TEGETA MADALE JUMAMOSI HII.....!!!!MAJINA MENGINE YATATAJWA KESHO MAPEMA.....!!!!ASANTE
… Read More
Madaha Ajikosha, Ampa Tano Makonda..!!..Fahamu zaidi hapa.
MWANAMUZIKI Baby Joseph Madaha amefungukia uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda wa kuanza kudili na wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya akisema kuwa, huenda ikasaidia mastaa wengi kubadilika. Akipiga stori na … Read More
0 comments:
Post a Comment