Mashabiki
takribani 58 waliotuma maoni yao kuhusiana na kikosi cha Yanga kwenye
blog hii, wamesisitiza kwamba kikosi chao lazima kijiimarishe katika
kiungo.
Mashabiki
hao wanaonekana kuingiwa hofu kutokana na kikosi hicho kupoteza mechi
dhidi ya Stand na kiungo kikionekana kimepwaya huku wakiwa wanakutana na
Simba, inayoonekana kuwa na kiungo bora zaidi.
Simba inaonekana kuwa na wachezaji wengi vijana zaidi na kiungo bora zaidi. Hali iliyoonyesha kuwapa hofu kubwa mashabiki hao.
"Hii
ni hatari sana, lazima kocha Pluijm aifanyie kazi. Unajua hawa jamaa
(Simba), wako vizuri sana katika kiungo," alisema Abdul Rashid wa
Buguruni jijini Dar es Salaam.
Paul
Matiku James wa Geita, naye alisema" "Stand walitupa shida kwenye
kiungo. Kilikufa kabisa, sasa tunakutana na Simba. Nina hofu sana."
Wengine walielezea kuhusiana na timu yao kutoonekana ina makali mbele kama ilivyozoeleka.
Hata hivyo, Kocha Hans van der Pluijm, tayari alishaueleza kwamba watahakikisha wanafanya mabadiliko kwa walichoona ni tatizo.
Tayari Yanga ipo mjini Pemba ikijiandaa na mechi dhidi ya Simba itakayopigwa Jumamosi ya Oktoba Mosi.
0 comments:
Post a Comment