Mwezi
mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni Ukuta kupinga inachokiita
ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia, leo
inatarajia kutoa mwelekeo wa mkakati huo.
Operesheni
hiyo ilipangwa kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na
mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya
chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni
pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara.
Siku
moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe alitangaza kuisitisha kwa mwezi hadi kesho, ili kutoa
fursa kwa viongozi wa dini kusemezana na Rais John Magufuli na Serikali
yake.
Jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema: “Kuhusu Ukuta, kesho (leo) tutatoa msimamo wetu juu ya kitu tutakachofanya.”
Alisema
operesheni hiyo ilisitishwa kutokana na sababu za msingi zilizoelezwa,
hivyo kauli ya chama hicho leo itafafanua kwa kina kuhusu mambo yote
yaliyojitokeza katika kipindi hicho cha mwezi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA, Tumain Makene alipost taarifa hii katika ukurasa wake;
CHADEMA, Tumain Makene alipost taarifa hii katika ukurasa wake;
Wakati
viongozi hao wakieleza hayo, hadi jana hakukuwa na taarifa zozote za
kufanyika kwa kikao kati ya viongozi wa dini na Serikali.
Viongozi
hao waliitaka Serikali na Chadema kufikiria amani ya nchi na kutafuta
njia mwafaka za kumaliza msuguano wa kisiasa hasa baada ya chama hicho
kushikilia msimamo wake wa kufanya mikutano na maandamano.
Wakati
Chadema wakijipanga kutoa tamko lao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda jana alisisitiza kuwa Oktoba mosi ni Siku ya Kupanda Miti
jijini humo ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria.
0 comments:
Post a Comment