KATIBU
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, atatua
ofisini kwa kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu,
ili kumueleza mkakati wake wa kutua ofisini kwake, Buguruni jijini Dar
es Salaam
Maalim
anakwenda kwa IGP Mangu kumueleza adhima yake ya kufika ofisi kuu ya
chama chake kesho Ijumaa, majira ya saa mbili asubuhi.
Hatua
ya Maalim kutinga ofisini kwa IGP imetokana na kitendo cha jeshi la
polisi kumsindikiza Prof. Lipumba kurejea ofisini; kusaidia uharibifu wa
mali na kushambulia wanachama na wafuasi wa chama hicho.
Azma
yake ya kwenda ofisini kwake kesho, inatokana na ofisi hiyo kuvamiwa na
aliyepata kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba na
genge la wafuasi wake.
Prof.
Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa CUF, 6 Agosti mwaka jana na miezi 11
baadaye akatangaza kurejea katika nafasi yake, amefukuzwa rasmi
uanachama wa chama hicho Jumanne iliyopita na Baraza Kuu la uongozi la
Taifa (BKT), lililokutana Visiwani.
Hata
hivyo, Prof. Lipumba, ameendelea kung’ang’ania kuwa bado mwenyekiti
halali wa chama hicho na msimamo wake huo, unadaiwa kuungwa mkono na
msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa watu waliokaribu na Maalim Seif zinasema,
kiongozi huyo amekwenda kwa IGP Mangu kumtaarifu kuwa yeye na wabunge wa
chama hicho, wamepanga kufika Buguruni kwa pamoja.
Anasema,
“Maalim Seif anakwenda kumweleza IGP Mangu kwamba, tayari kumekuwepo na
viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na watu wa Prof. Lipumba
na kwamba chochote kitakachotokea, yeye na jeshi lake, wanapaswa kubeba
msalaba.”
Prof.
Lipumba alijiuzulu uenyekiti karibu na uchaguzi mkuu mwaka jana,
akakimbilia nje ya nchi huku akidai hakufurahishwa na Edward Lowassa
kuwa mgombea urais chini ya mwavuli wa vyama vinne ikiwamo CUF.
Ukawa unaundwa na vyama vinne; Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na National League for Democrats (NLD).
0 comments:
Post a Comment