Muigizaji
wa Bongo Muvi, Steven Jacob ‘JB’ ambaye ni Simba ‘damu’, ametambia
kikosi chake kuwa lazima safari hii kilipize kisasi cha kufungwa na
Yanga msimu uliopita, huku akidai Yanga ikijitahidi itafungwa walau
kuanzia bao mbili kwenda juu.
JB,
nyota wa filamu ya Shikamoo Mzee, alifunguka sababu zinazompa jeuri
kuwa ni pacha kali ya Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo na Shiza Kichuya
ambayo imekuwa tishio tangu kuanza kwa msimu huu, akisisitiza kuwa bado
hajaona safu ya ulinzi yenye kuwazuia.
“Hata
wao wanalijua hilo kuwa hata siku moja Yanga haijawahi kucheza soka la
kueleweka mbele ya Simba, ni bahati tu iliwaangukia maana ni msimu
uliopita walifanya hivyo, siku nyingine walikuwa wakiogelea wao.
“Kwa
aina ya kikosi na ari ya wachezaji kwa sasa, sioni Yanga wanawezaje
kutufunga. Kasi ya washambuliaji Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo sijaona
beki wa Yanga wa kuweza kuwazuia,” alitamba JB.
Aidha,
JB alisema kuwa amepanga kuonana na wachezaji wa Simba kutoa ahadi yake
kuelekea mchezo huo ili kuwaongezea motisha wapate ushindi katika
mchezo huo utakaochezwa wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment