WAZIRI
MKUU Mhe. Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku 10 kwa Taasisi ya
Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu kulipa deni la sh. milioni 100
inayodaiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mafia.
Deni
hilo linatokana na malimbikizo ya miaka mitatu ya maduhuri yatokanayo
na makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo katika maeneo ya hifadhi ya
bahari wilayani humo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Ijumaa, Septemba 23, 2016 wakati
akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo katika ukumbi
Caltas akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi siku mbili.
“Waandikieni
barua na muitume leo hii kwa njia ya mtandao (email) kuwajulisha kuwa
wanatakiwa kulipa deni hilo ndani ya siku 10. Hakikisheni wanalipa deni
hili ili Halmashauri iweze kufanya kazi zake vizuri,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inataka kuona Halmashauri hiyo ikinufaika
kutokana na vyanzo vyake vya mapato, hivyo haitakuwa tayari kuona
ikihangaika.
Mbali
na agizo hilo, Waziri Mkuun amesema atafuatilia kuona wajibu wa taasisi
hiyo na mipaka yao ikiwa ni pamoja na kujua mapato yatokanayo na
shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.
Awali
mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema kuwa miongoni mwa
changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ni kutolipwa kwa wakati fedha za
maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na Taasisi ya Hifadhi ya
Bahari.
Mkuu
huyo wa wilaya ameiomba Serikali kuangalia upya majukumu ya taasisi
hiyo na nafasi ya halmashauri katika kuendesha shughuli za uwekezaji
pamoja na kupata mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya
hifadhi.
0 comments:
Post a Comment