Kikosi
cha Kilimanjaro Queens kimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na mashabiki na wadau mbalimbali
wa soka nchini.
Mashabiki
hao walijitokeza kwa ajili ya Kilimanjaro Queens ambaye wamekuwa ni
mabingwa wa Kombe la Chalenji la Cecafa baada ya kuwatwanga Kenya kwa
mabao 2-1 kwenye fainali mjini Jinja, Uganda.
Kina dada hao wa Tanzania Bara wameweka rekodi ya kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano ya Chalenji kwa wanawake.<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>
0 comments:
Post a Comment