Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Makonda Awaponda Wanaobeza Jitihada za Rais Magufuli, ‘Hawajui Wanalolitaka’.Fahamu zaidi hapa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemmwagia sifa Rais John
Magufuli kwa utendaji wake na kusema yeye ni mtu wa kutenda na sio
maneno huku akiwapa vidonge vya wale wanaobeza jitihada zake.
Makonda ametoa kauli hiyo Jumatano hii kwenye uzinduzi wa ndege mpya za
ATCL kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam.
“Mheshimiwa Rais naomba uendelee kutenda, sisi tumegawanyika kwenye
upande wa fikra,kuna watu ambao hawajui wanachokitaka na hata
ukiwafanyie yale ambayo ulifikiriA wao wanayataka kumbe sio,” alisema
Makonda.
“Ikumbukwe wakati wa bunge tulikuwa tunafuatilia kusikiliza, Tanzania
haina ndege tumezidiwa katika nchi za Rwanda tumezidiwa na wapi,
umenunua ndege wanaanza kusema ndege zenyewe hazijang’aa, wamekuja
kuzioshea airport, hawajui nini wanachokitaka. Hao hao walipiga kelele
tunataka elimu bure,angalau na wananchi wa hali ya chini wapate elimu
bure, wameanza kusema elimu yenyewe bure wakati majengo yanadondoka!
Kwahiyo hawajui wanalolitaka. Hawa hawa wana lalamika foleni Dar es
Salaam, umeamua kutujengea barabara hizo hela za barabara ingeenda
kwenye chakula tunakufa na njaa, mheshimiwa rais hawajui wanalolitaka,”
alieleza.
“Sisi tunaojua tunalolitaka tupo pamoja na wewe, tunakuunga mkono usiku
na mchana na tutaendelea kukuunga mkono usiku na mchana na ninaamini
kwamba wanasiasa wengi wanasubiri kutimiza ahadi zao katikati au
mwishoni mwa kuelekea kampeni wewe hujasubiri, uliahidi ndege mwaka jana
leo hata mwaka hujamaliza ndege zimeingia, wewe ni mtendaji ambaye
tutaendelea kukuombea,” alisisitiza.
Related Posts:
Kipini Cha Pua Cha Diamond chafanya Mashabiki watukanane mitandaoni.Fahamu zaidi hapa.
Watu wanahofia kipini cha pua cha Diamond kuliko hata kesho yao.
Kinachowaumiza zaidi mashabiki wake ni kuwa haoneshi kujali kilio chao.
Aliwashtua sana juzi pale alipoweka picha ikimuonesha akiwa na kipini
hicho na weng… Read More
Shamsa Amsweka Lupango Mzazi Mwenziye.Fahamu zaidi hapa.
STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford juzikati amemsweka lupango mzazi
mwenziye Dick Matoke, katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa kile
kinachodaiwa kuwa mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kumtukana mara
kwa mara akish… Read More
#YALIYOJIRI>>>>RAIS MAGUFULI AONDOA KIGOGO MWINGINE ILUKLU.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Kwa
mujibu wa mabadiliko yaliyotangazwa na Ikulu jana, Rais Magufuli
amemwondoa Ikulu Gelasius Byakanwa, ambaye alikuwa msaidizi wake wa
karibu.
Taarifa
ya iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisem… Read More
Radio EFM Yawachukua Watangazaji Gerald Hando na PJ...Imewatambulisha leo Rasmi.Fahamu zaidi hapa.
(PJ) pamoja na Abel Onesmo Jumamosi hii wametambulishwa rasmi EFM.Watangazaji wa zamani wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm, Gerald Hando, Paul JamesMkurungenzi wa EFM Radio, Francis Siza ‘DJ Majay’ (kushoto)… Read More
#YALIYOJIRI>>>Taarifa Ya CCM Kuhusu Kauli Ya Mhe Lowassa Kubeza Utendaji Wa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.Fahamu zaidi hapa.
Aliyekuwa
mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7,
2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya
ndani na nje ya nchi.
Katika
mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligu… Read More
0 comments:
Post a Comment