Thursday, 29 September 2016

#MICHEZO>>>>Yusufu Manji akabidhi ekari 700 zitakazojengwa Uwanja wa Klabu ya "YANGA" ufukweni mwa bahari ya Hindi, Gezaulole, Kigamboni.Fahamu zaidi hapa.

Jana Yusufu Manji kaikabidhi Yanga SC hekari 715 kujenga uwanja wa kisasa leo asubuhi hii MO kupitia ukurasa wa Simba SC ametangazwa kulipia kodi ya nyasi bandia zilizokwama kwa muda mrefu bandarini kumalizia ujenzi wa kiwanja cha mazoezi cha timu hiyo pale Bunju. 

Huu ndio ushindani wa jadi ambao vilabu hivi uliuweka kando kwa miaka mingi na kuzifanya kuwa masikini mwenye rasimali za kutosha . 


Natamani kusikia Azam FC nao wanaanza kujenga uwanja wao mkubwa wa kisasa au kuupanua uliopo angalau uweze kuingiza watazamaji 30,000. 


Mbeya City mna ushawishi mkubwa kuwateka wafanyabiashara wakubwa mkoani humo pia kutafuta wadhamini wa maana kujenga uwanja wa kisasa mkoani Mbeya . 


Ndanda FC piga goti kwa Dangote angalau uwanja mzuri kama wa Azam FC lakini si haba wafanyabiashara mkoani humo , wanasiasa maarufu wa mkoa huo hawashindwi kuwapa kiwanja angalau cha bilioni 1. 


Stand na Accacia Kambarage umechoka na wamiliki hawana dalili ya kuukarabati leo wala kesho . Katika udhamini wa bilioni 2 hebu toeni moja kwa kuanzia ujenzi wa kiwanja cha saizi ya kati ili kuondoa dhana ya viwanja vibovu mikoani .


Kila timu iwatazame kulwa na doto hawa katika dhana ya kujifunza kwa miaka mingapi wamepoteza muda na kushindwa kupata misuli sahihi ya kiuchumi kwa uwekezaji wa kisasa na nini wanafanya leo. 


Kuna timu hapa nchini ambazo kwa umri ni wakongwe sana kama zilivyo Yanga na Simba sema kwa sababu hazina ushawishi kitaifa hazitazamwi katika maendeleo ya kisoka kama walivyo Yanga na Simba . Hali hiyo na wao ina wapumbaza wanabaki kimya. 


Toto Afrika toka mwaka 1972 ! Coastal 1936 , Majimaji 1977 na African Sports 1938. Hawa wote watambue wapo nyuma kimaendeleo . Yawapasa kupata viwanja vyao . 


Timu zote zikiwa na fursa hii , ni dhahiri wigo wa ajira kupitia michezo utatanuka na hata masilahi ya nchi kwa misingi ya kodi itatanuka na mwisho siku maendeleo ya taifa kwa ujumla wake.


0 comments:

Post a Comment