Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>SERIKALI YATAKIWA KUPUNGUZA KODI VIFAA VYA INTERNET.FAHAMU ZAIDI HAPA.
SERIKALI imeshauriwa
kupunguza ushuru wa vifaa vinavyotumia intaneti ili kuongeza kasi ya
maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kijamii zinazotegemea huduma hiyo.
Wito huo umetolewa Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni inayotoa huduma za mitandao ya
Ericsson, Frode Dyrdal, wakati wa uzinduzi wa mitambo ya gharama nafuu
ya kusambaza intaneti.
Alisema huduma ya intaneti
inasaidia kuendeleza sekta za elimu, afya, fedha na burudani, hivyo ni
kiungo muhimu katika kuinua uchumi wa nchi.
“Wakati sisi tunajitahidi
kuhakikisha upatikanaji wa intaneti kwa gharama nafuu, ni vyema serikali
ikaangalia namna ya kuwafanya watu wengi wawe na vifaa vinavyotumia
intaneti na njia mojawapo ni kupunguza ushuru wa bidhaa za aina hiyo”,
alisema.
Alisema utafiti unaonesha kwamba ni watu wanne kati ya 10 ndio wanaoweza kupata intaneti barani Afrika.
Akizungumzia kuhusu mitambo
yao, alisema imelenga kutatua changamoto za upatikanaji mdogo, maendeleo
endelevu na gharama kubwa za huduma ya intaneti nchini.
0 comments:
Post a Comment