Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Prof.
Ibrahim Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF).
Jaji
Mutungi ameyasema hayo leo baada ya shauri hilo kufikishwa mezani kwake
siku kadhaa zilizopita kuhusu nafasi ya uenyekiti ndani ya CUF.
Awali
Prof. Lipumba ndiye alikuwa mwenyekiti, lakini alijiuzulu Agosti 2015,
mwezi Agosti 2016 chama hicho kikamteua Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti
wa muda hadi hapo uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti mwingine
utakapofanyika.
Lakini
Prof Lipumba alirudi na kusema yeye ndiye mwenyekiti halali wa CUF kwa
sababu barua yake ya kujiuzulu haikuwa imekubaliwa na Mkutano Mkuu wa
CUF.
Baada
ya mvutano wa muda mrefu ndani ya chama hicho, shauri hilo lilifikishwa
katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ambapo ametangaza rasmi kuwa
Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti.
Hapa chini ni maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
0 comments:
Post a Comment