Bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amekanusha uvumi
unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia akiwa nchini
Ujerumani.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa bilionea huyo amefariki akiwa nchini
Ujerumani baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aidha, taarifa hizo zinaeleza
kuwa familia ya bilionea huyo imethibitisha kifo cha ndugu yao huyo na
kusema kuwa ni pigo kubwa kwa Afrika.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dangote ameandika hivi “I am hale,
hearty and alive. Please disregard malicious report saying otherwise.
Thank you.” , akimaanisha kuwa yeye ni mzima wa afya na kuwataka watu
kupuuzia taarifa zinazoeleza kivingine.”
Akimaanisha “Mimi ni mzima na buheri wa afya. Tafadhali puuzeni taarifa zote zinazosema vinginevyo. Asanteni.”
0 comments:
Post a Comment