Mshambuliaji
Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk amefikisha mabao sita
ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubeligiji pamoja na mechi za Europa.
Katika
mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini
inaonekan Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho.
Kwani
katika mabao hayo sita, ni bao moja tu dhidi ya Oostende katika mechi
iliyochezwa Julai 31, ndiyo alifunga katika dakika ya 10.
Lakini
mabao mengine yote, amefunga kuanzia dakika ya 73 hadi 80, hali
inayoonyesha kuwa kila dakika 20 za mwisho, ni mtu wa kuchungwa kweli.
Mabao
aliyofunga katika mechi za Europa ni dhidi ya NK Lokomotiva, alifunga
katika dakika ya 83 na mechi ikaisha kwa sare ya mabao 2-2. Mechi ya
pili dhidi ya timu hiyo, akafunga pia katika dakika ya 80.
0 comments:
Post a Comment