KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25
maarufu kama panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao
maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini
Dar es Salaam.
Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua
wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi
hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Dar es Salaa jana mkazi wa
eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha kwa jina la Mwarami Abubakar
alisema hali sio shwari katika eneo kufuatia matukio ya kila siku ya
kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa mali zao na kundi hilo.
“Tayari vijana wawili wiki iliyopita wamechomwa moto na wananchi
wenye hasira huku mwingine akipigwa juzi hadi kutolewa utumbo na
kufariki papo hapo,” alisema Abubakar.
Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi
hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo mchana kweupe na wanatembea
kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za jadi kama nondo, visu na
mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni lazima wampige na kumpora.
Wenye maduka wanalazimika kufunga kuanzia saa moja jioni kuhofia
kundi hilo ambalo huvunja milango ya nyumba na kufanya uporaji” alisema
Fadhil.
Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi
(ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga vilivyokukabiliana na
vitendo hivyo katika mkoa wake.
“Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna kundi linalojiita panya
road wote tunawahesabu ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na hivi
ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita ya operesheni ya kukakamta
watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo wanaouza pombe
haramu ya gongo,” alisema Kamanda Hamdan.
Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi karibuni utakuwa shwari baada
ya askari wake kusambaratisha watu hao wanaofanya vitendo hivyo.
0 comments:
Post a Comment