Simba
imeikalia pabaya Yanga katika suala la beki Hassan Kessy na taarifa
zinaeleza kwamba, iwe isiwe, huenda Yanga inaweza kupoteza pointi katika
mechi zote ilizomtumia beki huyo.
Taarifa
zinaeleza, kamati iliyokuwa inalishughulikia suala hilo, imeona kuwa
Kessy alikuwa bado ana mkataba na Simba wakati akisaini Yanga.
“Kamati
imeona hivyo, imewaambia Yanga na Simba wakutane na kulimaliza. Mkataba
wa Kessy unatakiwa kuvunjwa kwa dola laki sita, Simba inaonekana
wamepiga mahesabu yao, wamepunguza hadi aslimia kumi ambaye ni dola elfu
sitini.
“Hizi
ni zaidi ya shilingi milioni mia ishiriki, si kidogo. Ndiyo maana
kamati imesisitiza Simba na Yanga wakae wao na kumalizana. Sasa utaona
hapa kuna shida.
“Yanga
lazima wawaangukie Simba, la sivyo mambo yatakuwa magumu kwao. Tena
katika mechi alizocheza Kessy au kukaa benchi, kama kamati itapitisha ni
batili au usajili wake una matatizo, pia watapokwa pointi.
“Nafikiri
aliyelishughulikia suala hili kama ni katibu wao, au kiongozi mwingine,
hakuwa mzuri katika masuala ya mpira. Atakuwa ni mgeni au si mtu makini
na ndiyo hivyo, Yanga sasa iko matatizoni katika hili,” kilieleza
chanzo cha uhakika.
Awali,
Simba ilisema iko tayari kumuachia Kessy lakini Yanga ilitakiwa
kuandika barua. Mwisho Yanga haikufanya hivyo, Simba ikaamua kulivalia
njuga, hata hivyo baadaye TFF ilimpitisha kuichezea Yanga.
0 comments:
Post a Comment