Thursday, 20 April 2017

Video:Wasanii wa Bongo Movie nchini waandamana Kariakoo – Dar.

DAR ES SALAAM: Baadhi ya wasanii wa Filamu nchini (Bongo Movie) wamefanya maandamano katika Mtaa wa Aggrey, Kariakoo ambapo ni sehemu maarufu kwa kuuza kazi za sanaa (CD za filamu mbalimbali) za ndani na nje ya nchi.

Wasanii hao wamefikia uamuzi huo ikiwa ni kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ya nchi ambazo wamedai kuwa zinaporomosha soko la filamu za ndani hivyo kusababisha kazi zao zisifanye vizuri sokoni.

Katika maandamano hayo wasanii wa Bongo Movie walisikika wakiimba.

“Movie za kikorea, Kihindi kwisha” wengine wakiitikia “Kwisha kabisa”.
“Hatutaki movie za nje, hatutaki movie za nje”
“Bai bai, bai bai, bai bai….”
“Uzalendo, uzalendo, uzalendo…”
Hayo yalikuwa baadhi ya maneno waliyokuwa wakiimba kuweka msitizo kuwa kwa sasa kazi zao ndiyo zinatakiwa zipewe kipaumbele ili sanaa iwanufaishe wasanii wa Tanzania na siyo vinginevyo.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment