Halmashauri
kuu ya chama cha mapinduzi CCM NEC imemaliza vikao vyake mjini Dodoma na
kutangaza majina ya wagombea wa nafasi za ubunge na uwakilishi katika majimbo
yote ya uchaguzi bara na visiwani watakao peperusha bendera ya chama hicho
katika uchaguzi mkuu ujao huku idadi kubwa ya majina ikiwa ni ya wabunge na
wajumbe wanaotetea nafasi zao za awali.
Kikao
hicho kilichokutana kwa siku mbili kikitanguliwa na kikao cha makati ya usalama
na maadili na kisha kamati kuu pamoja na mambo mengine kimepitia taarifa
mbalimbali pamoja na malalamiko ya baadhi ya wagombea sambamba na kupitisha
ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2015 huku majimbo 11 yakishindwa kupata
wagombea kutokana na sababu mbalimbali.
Mwaandishi alizungumza na baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu na wagombea waliopitishwa
kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi za ubunge kuhusu namna mchakato huo
ilivyoendeshwa ambapo wanakiri kulikuwa na changamoto kadha wa kadha huku
wakitaka mfumo huo uangalie namna na kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo
vilikuwa vikitajwa kugubika mchakato mzima.
Nao
baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma wanatoa maoni tofauti hukusu zoezi zima la
kuwapata wagombea wa nafasi za ubunge na uwakilishi kupitia CCM huku wakiwataka
kuwa na dhamira ya kweli ya uongozi na wasigeuze nafasi hizo za kuwawakilisha
wananchi kuwa ni ajira zao.
TOA MAONI YAKO HAPA.
0 comments:
Post a Comment