Thursday, 13 August 2015

#YALIYOJIRI>>>>Mgombea Urais kupitia Chadema UKAWA Edward Lowassa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.








Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa ameshindwa kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe hayati mzee Peter Kisumo yaliyokuwa yanafanyika Usangi mkoani Kilimanjaro baada ya msafara wake kuzuiliwa na polisi katika wilaya ya Mwanga kutokana na kuongozana na wananchi wakiwemo vijana waliokuwa na pikipiki waliokuwa wanakwenda kwenye mazishi.
Gari la Mh Lowassa ambaye pia ni mgombea urais wa Chadema akiwakilisha Ukawa lilianza kufuatwa na magari mengine ya watu binafsi na pikipiki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akitokea na Dar es Salaam na alipofika Moshi kundi la vijana walifunga barabara na kulazimika kuingia katika hotel ya kizi ambako pia walimfuata na kuzingira lango kuu na licha ya kuwasihi kuwa wampe nafasi aende kwenye mazishi vijana hao waliendelea kulifuata gara lake. 
Chanzo 
              ITV HABARI.

Katika hali ambayo sio rahisi kuamini vijana hao wakiwa na pikipiki waliendelea kufuata gari la Mh Lowassa hadi Mwanga na alipoanza safari ya kuelekea Usangi takrbani kilometa moja  kutoka barabara kuu polisi wakafunga barabara hali iliyosababisha mvutano mkubwa na jambo ambalo limelalamikiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti wa NCCR mageuzi James Mbatia na Mh Agustino Mrema.

Baada ya vuta nikuvute kati ya polisi na wananchi na viongozi hao wa vyama vya siasa mkuu wa polisi wa wilaya ya Mwanga aliruhusu watu waliokuwa na pikipiki kuendelea na safari kwa masharti ya kuondoa bendera za vyama vyao na pia kwenda bila msafara maelekezo ambayo licha ya kubalika utekelezaji wake ulikuwa mgumu na kusababisha kuendelea kwa malumbano na ndipo Mh Mbatia akata taarifa za Mh Lowassa kusitisha safari na kuamua kurudi Moshi na hatimaye Dar es Salaam.
TOA MAONI YAKO HAPA.

0 comments:

Post a Comment