Thursday, 2 June 2016

#BURUDANI>>> Huu ndo utambulishwa wa Rich Mavoko WCB hii leo.Fahamu zaidi hapa.

 Rich Mavoko akitia saini kuingia WCB.
Huu ndo utambulisho wa Rich Mavoko uliofanyika mbele ya waandishi wa habari hii leo.

A video posted by TANGAZA BIASHARA ZAKO HAPA. (@hebronmalele.blogspot) on

#YALIYOJIRI>>>>Wabunge 7 wa Upinzani Waliosimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge Waongezewa Adhabu.Fahamu zaidi hapa.

Wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni, watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.

Wabunge hao ambao Jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).

Adhabu hiyo ilitolewa  kama azimio la Bunge baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na kuomba mwongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi.

Habari zilizopatikana bungeni zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na Kanuni ya Bunge ya 75, ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa kazi.

Naibu Katibu wa Bunge (Shughuli za Bunge), John Joel alithibitisha kuwa utekelezwaji wa kanuni hiyo utafuatwa kwa wabunge wote ambao wamefukuzwa.

Akizungumzia hatua hiyo, Heche alisema hadi sasa hajapata barua ya kusimamishwa Bunge, hivyo hata kama watakata posho au mshahara haimsumbui kwa kuwa hawezi kusikitikia kitu hicho wakati haki inaminywa.

Zitto alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa barua inayoeleza mambo hayo wala ya kusimamishwa Bunge.

Nuh Mziwanda atoboa Siri ya ‘Jike Shupa’.Fahamu zaidi hapa.

Nuh Mziwanda amefunguka kile kilichojificha kwenye wimbo wake wa ‘Jike shupa’ ambao kwa sasa unafanya poa, aliomshirikisha Alikiba, na jinsi alivyoupokea kwa mara ya kwanza.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Nuh Mziwanda amesema Alikiba alimtaka Nuhu autoe wimbo huo bila yeye kutia sauti yake, kwani aliuona umekamilika na mzuri pia.

“Kiukweli nilikuwa nishaurekodi ushaisha, na nilikuwa nina plan ya kuuachia mimi mwenyewe, baadae nikaona mbona nimekaa kimya muda mrefu alafu nahitaji kuja kitofauti, ndio nikamfuata Alikiba nikamsikilizisha, nashukuru Mungu mwenyewe aliupenda kwa muda mfupi, akaniambia Nuh mbona wimbo umekamilika? uachie tu hivi hivi, nikamwambia hapana nahitaji sauti yako, ndio maana Kiba kaimba kidogo sana lakini kafanya kitu kikubwa”, alisema Nuhu Mziwanda.

Pia Nuhu Mziwanda amesema anaamini wimbo huo utakuja kubadilisha status yake na kuwa kubwa zaidi kuliko alipo sasa , kwenye kazi zake za muziki.

eatv.tv

Snura Amkabidhi Jipu Mama Samia.Fahamu zaidi hapa.

STAA wa muziki Bongo, Snura Mushi ameibuka na kumkabidhi Makamu wa Rais, Samia Suluhu jipu la wanaume wanaowakataa watoto wao na kuwaachia wanawake mzigo wa kulea peke yao.
Snura Mushi

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Snura alisema siku hizi wimbi la wanaume kuwakataa watoto wao ni kubwa sana hivyo tatizo hilo ni sawa na majipu mengine, anamuomba mama Samia alitumbue.

“Namuomba mama Samia kwa sababu ni mwanamke mwenzetu atusaidie kulitumbua hili jipu maana ni kubwa sana yaani tena ni tambazi kabisa, kama rais anavyowatumbua watu naye atumbue hili maana wanawake tumechoka.

“Nina watoto wawili lakini baba zao wamenisusia, wa kwanza alimkataa tangu nikiwa na mimba ya wiki mbili mpaka sasa nalea mwenyewe, huyu mwingine hajawahi kutoa chochote tangu mwanaye huyu azaliwe kitu ambacho kinaumiza sana,” alisema Snura.

Aliendelea kusema kuwa baada ya mama Samia kutumbua hilo jipu anaomba serikali iweke sheria ya kwamba kila kituo cha polisi kiwe kinapokea malalamiko ya wanawake wanaosusiwa watoto au mimba ili shtaka linapokwenda waandikishane na baada ya mtoto kuzaliwa ikigundulika mtoto ni wa mwanaume husika alipishwe fidia.

“Pia kipimo cha DNA kiwepo katika hospitali mbalimbali ili iwe rahisi kupima kwa wale wanaume wanaokataa kwamba watoto siyo wao, sheria hizi zikiwekwa zitasaidia kutokomeza tatizo hilo la watoto kukataliwa na baba zao,” alisema Snura.

Jitihada za kuzungumza na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kujua ameipokeaje changamoto hiyo, hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.

Snura ni mama wa watoto wawili kila mmoja na baba yake ambapo anawalea mwenyewe huku akikiri kwamba huwa anawaeleza wanaye hao jinsi baba zao walivyowakataa ili baadaye kusije kutokea mvutano wa kimasilahi pindi watakapofanikiwa.

Chanzo:GPL

#YALIYOJIRI>>>Update: Wabunge Wote Wa Upinzani Watoka Nje Asubuhi Hii Kupinga Naibu Spika Kuendesha Vikao vya Bunge.Fahamu zaidi hapa.

Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena  wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje  majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Kambi  upinzani  ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale "haki itakapopatikana."


#YALIYOJIRI>>>>JWTZ Yajitosa Mauaji Ya Watu 8 Tanga.Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange Atangaza Msako usiku na Mchana.Fahamu zaidi hapa.

SERIKALI imetuma kikosi maalumu cha ulinzi, kikiongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuwasaka watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao wanaendesha mauaji ya kinyama mkoani Tanga.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya watu wanane kuuawa kinyama kwa kuchinjwa juzi usiku katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Manispaa ya Tanga.

Habari za uhakika ambazo tulizipata jana, zinasema tayari vikosi hivyo vimeanza operesheni kali katika mapango ya Amboni ambayo yanadaiwa kuwa maficho ya watu hao.

Akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi ya marehemu wanne kati ya wanane waliozikwa Kibatini jana, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema vyombo vya dola vitahakikisha watu wote waliohusika katika mauaji hayo wanatiwa mbaroni.

“Ndugu zangu nawapeni pole kutokana na kuondokewa na wapendwa wetu… naomba kuwahakikisha sisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola tutahakikisha tunawatia nguvuni watu wote waliohusika na mauaji haya,” alisema Jenerali Mwamunyange.

Alisema tukio la mauaji hayo ni la kusikitisha mno kutokana na Tanzania kusifika kuwa nchi ya amani duniani.

“Tanzania inasifika kuwa na amani duniani kote, lazima hatua za kiusalama zichukuliwe haraka ili kunusuru amani yetu isichezewe.

“Ni tukio la ajabu ambalo limegusa watu wengi wasio na hatia, tutasaidiana na wenzetu kuhakikisha wahalifu hawa wanapatikana,” alisema Jenerali Mwamunyange.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Masauni Hamad Masauni, alisema Serikali inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo ili kuwakamata wahusika ndani ya kipindi kifupi.

Aliwahakikisha wananchi kuwa ulinzi unaimarishwa na kwamba matukio hayo hayatajirudia tena.

“Vyombo vya ulinzi vitafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha tunawatia nguvuni haraka watu waliohusika na mauaji hayo,” alisema Masauni.

Aliwaomba ndugu na jamaa ambao wamefiwa na ndugu zao kuwa na subira wakati Serikali inaendelea kuchukua hatua.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu alisema wataendelea kuimarisha ulinzi na usalama maeneo yote.

Katika hatua nyingine, wakazi wa mitaa mitatu ya Mleni Kati, Mleni Mashariki na Kibatini katika Kata ya Mzizima, Manispaa ya Tanga, wameanza kukimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wao baada ya mauaji hayo.

Mauaji hayo yalitokea juzi usiku ambapo watu wanaoaminika kuwa majambazi walivamia nyumba tatu katika eneo hilo, wakiwa wamelala usiku, kisha kuwateka na kuwapeleka msituni kabla ya kuwachinja.

Wakazi hao wanaounda zaidi ya kaya 30, walisema wameamua kuyakimbia makazi yao kwa kutokuwa na imani ya usalama wao katika eneo hilo, baada ya wale wanaoitwa majamabzi kuvamia makazi yao kwa mara ya pili kwa staili ya kutisha.

Kabla ya tukio hilo la juzi, watu wasiofahamika walivamia makazi yao na kuchinja kuku 40, mbuzi wanne na ng’ombe mmoja na kukimbilia mapango ya Amboni na hawajawahi kukamatwa.

Mwandishi wetu  jana  alishuhudia wanawake na watoto wakiwa na mizigo mithili ya wakimbizi wakiondoka katika eneo hilo huku wanaume wakibaki kwa ajili ya kuzika ndugu, jamaa na marafiki zao waliouawa katika tukio hilo.

Mmoja wa wananchi hao, Juma Issa, alisema wamelazimika kuwahamisha wanawake na watoto kwa kuhofia wanaweza kuvamiwa tena kwa mara ya pili.

Nae Lucas Muhina alisema kuwa anashindwa kuhama katika eneo hilo kutokana na kuwa na mifugo, hivyo anashindwa kujua mahali salama pa kuihifadhi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibatini, Shabani Mwamini, alithibitisha baadhi ya wananchi wa mitaa mitatu kuhama katika eneo hilo.

“Nyumba nyingi zimebaki na wanaume pekee yake kwani wanawake na watoto wote wamehama kwa sasa,” alisema.

Wakati huohuo, maiti nne kati ya nane zimezikwa jana huku nyingine nne zikisafirishwa nje ya mkoa huo.

Mwamini aliwataja waliozikwa kuwa ni Issa Husein, Mkola Husein, Issa Hamis na Salim Adam.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella alisema kuwa vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Simulizi ya Mauaji
Mtoto wa marehemu Mkola Hussein anayeitwa Salimu Mkola (16) alisababisha vilio na simanzi kwa waombolezaji baada ya kusimulia namna watu hao walivyomchukua baba yake na kwenda kumchinja mbele ya nyumba yake.

Akisimulia tukio hilo huku akibubujikwa machozi, mtoto huyo alisema watu hao walifika nyumbani kwao wakagonga mlango saa sita usiku na kumuamrisha baba yao atoke na fedha.

“Nilipoona hivyo nilijaribu kupiga kelele kuomba msaada kwa majirani, lakini mmoja wa wauaji aliingia ndani na kunitoa nje ya nyumba yetu, huku akiniuliza wakati wale vijana saba
wanachukuliwa na polisi mimi nilikuwa wapi.

“Waliendelea kuniuliza kama nina habari ninayoijua, huku wakiwa wameshika mapanga na bunduki, ndipo waliponiambia wapo kwa ajili ya kutetea dini yetu.
 
“Baadaye waliniruhusu niingie ndani na kulala, lakini niliendelea kusikia vishindo vya kipigo na watu wakikoroma ambayo ilikuwa ni ishara ya kuwa baba yangu alikuwa anakata roho pamoja na watu wengine,” alisema.
 
Mtoto mkubwa wa marehemu, Abuu Mkola, alisema vijana saba ambao sasa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi awali walionekana katika Kitongoji cha Kibatini wakiwa wanakimbia kusikojulikana.

Alisema baada ya hali hiyo baba yake ambaye ni marehemu, Mkola Hussein akishirikiana na wananchi wa mtaa huo walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambao walikuja na kuwakamata vijana hao lakini mmoja wao alifanikiwa kukimbia.
 
Abuu alisema kuwa katika tukio la juzi, wauaji hao wakati wanamchukua baba yake walisema wanawahitaji vijana wao saba waliokamatwa na polisi, lakini aliposema hajui ndipo walimuunganisha na watu wengine kwa ajili ya kumchinja.

Bunge Lataka Taarifa
Ofisi ya Bunge imeiagiza Serikali kutoa taarifa rasmi kuhusu mauaji yanayoendelea nchini ili kuwatoa hofu wananchi waliopo katika maeneo mbalimbali.

Akitoa maagizo hayo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alisema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni anapaswa kuzungumza na Kamati za Ulinzi na Usalama katika maeneo yote ambayo yametokea mauaji ili aweze kutoa taarifa ndani ya Bunge.

“Waziri atuletee taarifa kwa sababu Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo hapa na waziri anayehusika na mambo ya Bunge yupo, naomba watuletee taarifa kwa sababu mauaji yamekuwa yakitokea mara nyingi na tumekuwa tukiwasihi Serikali ituletee taarifa na si mtakuwa mnazitafuta,” alisema Dk. Tulia.

Baada ya maelezo hayo Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) alisimama na kuomba mwongozo chini ya kanuni 68 (7).

“Mheshimiwa Naibu Spika pamoja na haya uliyoyatolea maelezo juu ya mauaji yanayotokea katika nchi yetu, nimelazimika kuomba mwongozo huu kwa sababu matukio yaliyoanza kujitokeza katika maeneo mbalimbali na maeneo mengine mambo haya tuliwahi kuyauliza Serikali na kuahidi watayatolea ufafanuzi.

“Sasa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani  amekwenda kuangalia na atazungumzia jambo hilo wakati mambo haya wabunge tulishaiomba Serikali itoe ufafanuzi ni jinsi gani inajipanga kukabiliana nayo,” alisema Lugola.

Alisema kitendo cha Serikali kusema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amekwenda kushughulikia jambo hilo wakati huo huo mambo ambayo yametokea Mwanza na maeneo mengine yalishaombewa ufafanuzi lakini hakuna majibu si kizuri.

#YALIYOJIRIBUNGENI: Kambi ya Upinzani imewasilisha hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye hii Leo.Fahamu zaidi hapa.

Wabunge wa upinzani wamewasilisha kwa Spika wa Bunge hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa kutokuwa na imani naye.

Hatua hiyo imefikiwa na wabunge hao kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa uongozi wa Dk Tulia anapokalia kiti cha Spika.

Tangu Jumanne wiki hii, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo kwa madai anaminya demokrasia.

Walifikia uamuzi huo baada ya Dk Tulia kuzuia kujadiliwa hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi zaidi ya 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) iliyowasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na kukatisha mjadala wa bajeti ya maji.

Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wote wa upinzani kupingana na maamuzi ya Dk Tulia, jambo lililosababisha watolewe bungeni.

Kutokana na hali hiyo wabunge hao kupitia Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya akisindikizwa na Mbunge wa Kibamba, John Myika wa Chadema na Mbunge wa Konde wa CUF, Khatibu Said Haji waliwasilisha hoja hiyo kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah baada ya Spika, Job Ndugai kutokuwapo bungeni.

Hoja hiyo iliwasilishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 138 (1) ambayo inaeleza utaratibu wa jinsi ya kumwondoa Naibu Spika.

Kanuni hiyo inasema, “Utaratibu wa kumwondoa Naibu Spika madarakani chini ya Ibara ya 85(4)(c) ya Katiba utakuwa kama ule wa kumwondoa Spika, isipokuwa tu taarifa ya kusudio la kumwondoa Naibu Spika madarakani inayoeleza sababu kamili za kuleta hoja hiyo, itapelekwa kwa Spika ambaye ataiwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuijadili.”

Fasili ya pili ya Kanuni hiyo inasema: “Endapo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Naibu Spika zinazohusu uvunjaji wa Katiba, Sheria au Kanuni zinazoongoza Shughuli za Bunge, basi Kamati hiyo itaidhinisha kuwa hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.”

Kwa mujibu wa Ibara ya 85(4)(c), Naibu Spika atakoma kuwa Naibu Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika endapo ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu Spika kwa azimio la Bunge.

Akizungumzia uwasilishwaji wa hoja hiyo, Millya alisema taarifa zaidi watatoa leo kuhusu msimamo wao huo.

Dk Tulia aliwataka wabunge wenye malalamiko juu ya utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za Bunge kukata rufaa kwa kufuata Kanuni za Bunge.

Alisema kanuni ndogo ya 5(2) inasema Spika atawajibika kutilia nguvu kanuni zote za Bunge na 5(3) inasema Spika anaweza kumtaka mbunge yeyote anayekiuka kanuni hizi kujirekebisha mara moja.

Alisema kwa hiyo mbunge yoyote asiyeridhika, kanuni za Bunge zinamruhusu kukata rufaa na zinamweleza nini cha kufanya.

Wednesday, 1 June 2016

#YALIYOJIRI>>>Serikali Yatoa Ufafanuzi Uboreshaji wa Maslahi ya Polisi na Nafasi za JKT.Fahamu zaidi hapa.

Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi na kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha maslahi ya Askari wa Jeshi hilo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni mjini Dodoma leo
 
Amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza Mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za Polisi 4136 ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Polisi.

Amesema Serikali imechukua hatua za haraka kulishughulikia suala la ukosefu wa nyumba za askari hao katika maeneo mbalimbali nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye ukosefu wa nyumba hizo.

Amelieleza Bunge kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Askari Polisi yanaimarishwa ikiwemo malipo ya Posho ya pango kwa askari wasio na nyumba ambayo ni asilimia 15 ya mishahara yao ili waweze kulipia gharama hizo.

Ameongeza kuwa  askari wenye utalaam maalum wakiwemo madereva na madaktari wamekuwa wakilipwa posho ya asilimia 15 ya mishahara yao na kuongeza kuwa askari wanaoajiriwa katika ajira mpya kama madaktari wamekuwa wakilipwa mishahara sawa na madaktari wengine bila kujali vyeo vyao.

“Serikali tumefanya jitihada kubwa sana kuboresha maslahi ya askari wetu, kama Serikali tumetoa posho za nyumba, posho za utalaam maalum kwa askari wote ambayo ni asilimia 15 ya mshahara wa kila Polisi hii yote ni kuwafanya askari wetu waweze kumudu gharama za maisha” Amesisitiza Mhe. Mpina.
 
Ameeleza kuwa kwa askari wanaofanya kazi katika mazingira magumu wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamekuwa wakipewa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (Hardship allowance) kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kila mwezi.
 
Mhe. Mpina amebainisha kuwa askari wote wanaohitimu mafunzo yao wamekuwa wakikatiwa Bima ya Afya kwa asilimia 100 na Serikali pamoja na udhamini wa mikopo mbalimbali katika taasisi za kifedha ili waweze kupewa mikopo na taasisi hizo.
 
Aidha, amesisitiza kuwa serikali imewapandishia kiwango cha Posho ya katikati ya mwezi (Ration Allowance) kutoka shilingi 180,000 za awali hadi 300,000 ambazo wanalipwa kwa sasa nchi nzima.
 
Katika hatua nyingine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imetoa ufafanuzi kuhusu vijana wa kidato cha nne kutochukuliwa kujiunga na  Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi  amesema kuwa hatua ya kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kwa sasa haiwezekani kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali.
 
Amesema kuwa uwezo wa JKT kuchukua vijana wa kujitolea kwa sasa ni 5000 hadi 7000 kwa mwaka kulingana na bajeti inayotolewa na kuongeza kuwa mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha na kujenga kambi zaidi za mafunzo ili kuwawezesha vijana wengi kujiunga  na mafunzo hayo kulingana na upatikanaji wa fedha.
 
Kwa upande wa wahitimu wa kidato cha sita wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria Mhe. Mwinyi amesema Serikali imewachukua vijana 14,000 na inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kuchukua vijana wengi zaidi.
 
Amesema Serikali inakusudia kujenga majengo ndani ya makambi ili kuwezesha vijana wote wanaohitimu kidato cha sita kupitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.
 
Aidha, Amefafanua kuwa kwa wale wanaojiunga na JKT kwa kujitolea ambao idadi yao inafikia 5000 sio wote wanaopata nafasi ya kuajiriwa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuongeza kuwa ni asilimia 71 ndio hupata ajira kwenye vyombo hivyo huku waliobaki wakilazimika kurudi nyumbani.
 
Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaangalia utaratibu wa kuwawezesha vijana hao ili wanaporudi uraiani waweze kupatiwa mitaji ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe.

#YALIYOJIRI>>>>NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MSITU WA MAPANGOPORI YA AMBONI.Fahamu zaidi hapa.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akizungumza katika Kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigella. Watatu kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (wapili kushoto). Viongozi hao wamekutana  mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia), mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella kabla ya kwenda katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI.

#YALIYOJIRI>>>>Wabunge waliosimamishwa watoa ya Moyoni.Fahamu zaidi hapa.

Bungeni Dodoma 

Wakiongea kwa nyakati tofauti Mjini Dodoma, Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa ni dhahiri wasiwasi waliokuwa nao toka awali unajidhihirisha wazi kuwa bunge hilo litakua ni kibogoyo na kukosa maamuzi.

Nae Mbunge wa Bunda Mhe. Esther Bulaya amesema lengo kuu la adhabu iliyotolewa dhidi yao ni kutaka kupunguza nguvu ya upinzani bungeni pamoja na kutaka kuwatisha wabunge washindwe kuwawakilisha wananchi wao ipasavyo.

Kwa upande wake Mbunge aliesimamisha kwa vikao Kumi mfululizo Mhe. John Heche amesema hata kama atarejea ndani ya bunge hilo ataendelea na misimamo yake ya kutetea wananchi bila woga kwa kujali maslahi ya taifa.

Hati hivyo Baraza la Vijana la Chama cha Demkorasia na Maendeleo CHADEMA wamelalamikia kitendo hicho huku wakimtaka Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson ajipime mwenye kama anafaa kuendelea kuliongoza bunge hilo huku Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC),Hellen Kijo Bisimba akisema hatua hiyo imewanyima haki wananchi kwa wabunge waliowachagua.

Msanii mkongwe Jay Moe asema ukimya wake umemfanya ajue wasanii wenzake huwaga wanakosea wapi.Fahamu zaidi Bofya hii link hapa.

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Jay Moe amesema ukimya wake kwenye game la muziki umemfanya ajue wasanii wenzake huwaga wanakosea wapi.
Rappa huyo ambaye amedai amekaa miaka 4 bila kutoa ngoma yake binafsi, ameiambia Bongo5 kuwa amegundua style mpya ambavyo itamfanya afanye vizuri zaidi.

“Unajua kuna kitu fulani kama malaika anakwambia acha hiki fanya hiki, alafu kweli unakifanya na unaona kabisa leo kinaleta manufaa, nimejifunza vitu vingi sana, sasa hivi wasanii wenzangu wanakuja na nyimbo mpya sometime nakuta nacheka, naona mbona nyimbo hii bado haipo kwenye muziki wa siku hizi. Hii time ambayo nilikuwa nje ya muziki nimejikuta nimesoma vitu mpaka vilivyo mbele yangu,” alisema Jay Moe

Aliongeza, “Pia ukimya wangu nilikuwa napanga mambo mengine nje ya muziki, hatuwezi tukafocus kwenye muziki tu, tumeshakuwa watu wazima wengine, huko tunakoelekea tutafanya muziki labda miaka 4 tu. Hatuna muziki wa Marekani wa kuona akina Dr Dre bado wananufaika kazi zao mpaka leo,” alisema Jay Moe.

Jay Moe amesema anajipanga kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Pesa ya Madafu’.

#YALIYOJIRI>>>Utafiti: Mbwa kuwa tiba ya Malaria.Fahamu zaidi hapa.

Kemikali zinazopatikana katika watu walioambukizwa ugonjwa wa Malaria zinaweza kutolewa na mbwa ,utafiti umebaini.

Wanasayansi katika shule ya London kuhusu usafi na dawa kutoka eneo la tropiki wamepewa takriban dola 100,00 na wakfu wa Bill and Melinda Gates ili kufanya utafiti zaidi.

Watashirikisha usaidizi kutoka watoto 400 wa Gambia,ikiwemo baadhi ambao wanajulikana kuwa na ugonjwa wa Malaria ambao watahitajika kuvaa soksi za nailoni kwa saa 24.

Mbwa hao watafunzwa kubaini kati ya violezo vya malaria na vile ambavyo sivyo.
Mmoja ya watafiti James Logan aliambia BBC Newsday kwamba hatua hiyo itasaidia kuzuia kusambaa kwa Malaria.

Chanzo
            BBC SWAHILI.

#YALIYOJIRI>>>ZITTOKABWE:Kukubali kufanywa vikaragosi vya viongozi ni dalili ya woga.Fahamu zaidi hapa.

 
Hiki ndo alicho kisema Zittokabwe kwenye ukulasa wake wa Instagram"Kukubali kufanywa vikaragosi vya viongozi ni dalili ya woga, si dalili ya heshima; na woga na heshima ni vitu viwili mbali mbali. Maadili mema hayatudai tuwaogope viongozi wetu. Na viongozi makini hupenda kupata heshima ya wananchi wenzao, lakini hawapendi kuogopwa. Kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta, viongozi halisi hawapendi kuishiriki. Kujenga mazoea ya kutii viongozi hata katika mambo haramu ni dalili ya woga, ni kukaribisha udikteta"

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA...MWL J.K.NYERERE.

 

Rose Ndauka:Ahadi yangu ipo pale pale.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa Filamu bongo Rose Ndauka
 
Akizungumza na eNewz Rose alisema kuwa yeye hajashindwa kufanya hivyo kwa kuwa tayari anawasanii ambao wameshawasajili wakiwa na nyimbo zao tayari na kudai kuwa yeye peke yake hawezi kwakuwa hafahamu kitu kuhusu muziki lakini kwa kusaidiana na wataalamu ambao yupo nao watakamilisha tu hivi karibuni 

Aidha, Rose aliweza kutoa maoni yake kuhusiana na kauli iliyokuwa imetolewa na nguli wa filamu nchini Bibi Hindu dhidi ya wasanii wa kike wa Bongo movie kuhusu uvaaji wao wa nusu uchi mpaka kufikia filamu kushindwa kuangaliwa na watoto wakiwa na wazazi wao,

"Hakuna shida mtu kuvaa kimini kama mtu ana mguu unamruhusu kuvaa hivyo inategemea na uhusika tu wako tu na pia filamu zinaandikwa kabisa kuwa hii inaangaliwa na wote na hii hairuhusiwi kuangaliwa na mtoto wa chini ya miaka kumi nane kwanini sasa watoto waangalie,” alihoji Rose Ndauka.

#YALIYOJIRI>>>>Rais Magufuli amteua Dr. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanoa Dr. John Pombe Joseph Magufuli leo tarehe 31.05.2016 amemteuwa Dr Alex L. Kyaruzi kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO).
Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati Prof Sospeter Muhongo amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania ( TANESCO) kuanzia tarehe 31.05.2016 hadi tarehe 30.05.2019

1.Dkt. Samwel Nyantahe
2.Dkt. Lugano Wilson
3.David Elias Alal
4.Mhandisi Stephen Peter Mabada
5.Mhandisi Leonard R. Masanja

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Kuanzia tarehe 31.05.2016 hadi tarehe 29.05.2019

**Abdalah H. Musa
**Dkt. Coretha Komba
**Felix M. Maagi
**Dkt. Lightness Mnzava
**John B. Seka

Aidha imeelezwa kuwa uzinduzi wa bodi hizi utafanyika makao makuu ya mashirika haya tarehe 02.06.2016 siku ya Alhamis saa 4:00 asubui kwa STAMICO na Saa 8:00 Mchana kwa Tanesco.

#YALIYOJIRI>>>>Magufuli: Serikali Itakomesha Watumishi na Wanafunzi Hewa.Fahamu zaidi hapa.

RAIS John Magufuli (pichani) amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kumaliza makosa yote yaliyojitokeza huko nyuma ikiwemo tatizo la watumishi na wanafunzi hewa lililoibuka hivi karibuni.

Amewataka Watanzania kuacha kuingiza siasa kwenye makosa yanapojitokeza, hasa yale yanayogusa sehemu nyeti kama elimu, kwani yakiachwa kuna uwezekano wa kutengeneza taifa la watu wa ajabu.

Alisema tangu aingie madarakani amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwemo matatizo ya rushwa, ukwepaji kodi, watumishi hewa na sasa amekumbana na tatizo la wanafunzi hewa.

“Nchi yetu ina changamoto na mambo mengi sana hata mimi nimekumbana na changamoto naziona mwenyewe, nikigeuka hivi watumishi hewa ambao hadi sasa wamefikia 10,500, nikigeuka hivi kuna wanafunzi hewa,” alisisitiza.

Alisema ni Tanzania pekee ambayo mtu anaweza kupata daraja la nne kidato cha nne katika elimu ya sekondari, halafu akapata fursa ya kujiunga na chuo kikuu na kupatiwa mkopo wa serikali, wakati mhitimu aliyefaulu kidato cha sita akikosa fursa hiyo.

Alisema endapo kulifanyika makosa lazima yarekebishwe, kwani inafahamika fika mtu akimaliza kidato cha nne akifeli ataanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada ndio apate nafasi ya kujiunga chuo kikuu.

“Sasa hapa kwetu ni tofauti ukifeli kidato cha nne unajiunga chuo kikuu,” alihoji na kuwataka watu waache siasa kwenye makosa kwani mambo kama hayo yakiachwa kuna hatari ya nchi kutengeneza taifa la ajabu.

Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako aliivunja Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na kuwasimamisha kazi viongozi wanne waandamizi kwa tuhuma za kudahili wanafunzi wasio na sifa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Awadh Mawenya naye alisimamishwa kazi kwa kosa la kushindwa kuwachukulia hatua watumishi waliodahili wanafunzi hao wasio na sifa. 

Profesa Ndalichako alichukua hatua hizo baada ya TCU kudahili wanafunzi 489 waliopata daraja la 4.32 katika mitihani yao ya kidato cha nne lakini walijiunga na chuo kikuu na kupatiwa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 784.

Picha: Harmonize Amtambulisha Wolper Ukweni.Fahamu zaidi hapa.

Wikiiliyopita staa anaechipukia kwenye bongo fleva Harmonize alimpeleka mpenzi wake Jacqueline Wolper kwao Mtwara alikoenda kutumbuiza kwa mara ya kwanza tangu aukwae ustaa kupitia label ya WCB.
“Time Ya Kumsaidia mama Harmo Kuanda Chakula Cha Usiku Mtwara Life @wolperstylish,” aliandika Harmonize kwenye picha inayomuonesha Wolper akichuma matembele shambani.
Wolper akiongea na mama yake Harmonize

Naye Wolper alipost picha akiwa na mama mkwe na kuandika: I am having the best time of my life.. Nikiwa na Mama angu… Kabla hamjatoka lazima mpige story, akuchekeshe… Mjipikilishe.. Akushauri

Hapa nimepata rafiki kwa kweli…I love my mama Mkwe.. Mama Raj wangu.”


Bongo5