Wabunge
wote wa vyama vya upinzani leo tena wametoka nje kupinga Naibu Spika
wa Bunge Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge
yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa
kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje
kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na
imani na Dk Tulia.
Baada
tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje majira
ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.
Kambi upinzani ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.
Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema
wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale
"haki itakapopatikana."
0 comments:
Post a Comment