JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
• WATU
NANE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA NA POMBE AINA
YA GONGO KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MAENEO YA LUCHELELE WILAYANI
NYAMAGANA.
KWAMBA
MNAMO TAREHE 16.06.2016 MAJIRA YA SAA MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA
ENEO LA LUCHELELE WILAYA YA NYAMAGANA MKOA WA MWANZA, ASKARI POLISI
WALIFIKA KATIKA ENEO HILO TAJWA NA KUFANYA MISAKO PAMOJA DORIA NAKUWEZA
KUFANIKIWA KUKAMATA WATU NANE WAKIWA NA POMBE AINA YA GONGO PAMOJA
NAMITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA
SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
WATUHUMIWA
WALIOKAMATWA, 1. JESCA SIMONI MIAKA [14], MWANAFUNZI, AMBAYE ALIKAMATWA
AKIWA NA LITA 42 ZA POMBE AINA YA GONGO, 2.NYANGE BIHEMO MIAKA [46]
ALIYEKAMATWA AKIWA NA MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 3.
MARIAM OMARY MIAKA [28] ALIYEKAMATWA NA POMBE YA GONGO LITA 3, 4.
MAOLA
LUCHUPA MIAKA 32 ALIYEKAMATWA AKIWA NA LITA 20 ZA POMBE AINA YA GONGO.
WENGINE NI, 5. ELIZABETH JOHN MIAKA 35 ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MITATU YA
KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, 6. ANASTAZIA ALOYCE MIAKA 25 ALIYEKAMATWA
NA POMBE YA GONGO LITA 2, 7. TEDY PIUS MIAKA 40 ALIYEKAMATWA NA LITA 30
ZA POMBE YA GONGO NA, 8. PASKAZIA THOMAS ALIYEKAMATWA NA MITAMBO MIWILI
YA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO, WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA LUCHELELE.
AIDHA
INADAIWA KUWA WATUHUMIWA HUFANYA BIASHARA HARAMU YA POMBE YA GONGO NA
WAKAZI WA MAENEO HAYO, HUKU WAKIIHALALISHA BIASHARA HIYO KUWA KAMA
CHANZO CHAO KIKUU CHA KIPATO CHA KILA SIKU KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI
WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI. NDIPO JESHI LA POLISI LILIPOKEA TAARIFA
ZA KIINTELEJENSIA KUHUSIANA NA UHALIFU HUO UNATENDWA NA BAADHI YA WAKAZI
WA LUCHELELE NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU.
WATUHUMIWA
WOTE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA
UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE AINA YA
GONGO UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI
KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA
WAFANYE KAZI NYINGINE HALALI AMBAZO ZITAWAINGIZIA KIPATO, LAKINI
BIASHARA HARAMU ZA POMBE YA GONGO NA MADAWA YA KULEVYA NAWAOMBA MUACHE
KUJIHUSISHA NAZO KABISA, KWANI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA
LIMEJIPANGA VIZURI KUKABILIANA NA WAHALIFU WA AINA KAMA HIYO NA
KUHAKIKISHA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA.
0 comments:
Post a Comment