Waziri
mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya
kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika Muungano
wa Ulaya (EU).
Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo ang’atuke.
Waziri
Mkuu huyo aliyeongoza kampeni ya kusalia katika muungano wa EU amesema
kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri
duniani.
Akiongea
katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London,
Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa
hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Sauti yake iliibua hisia hasa aliposema "nalipenda sana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote."
Cameron
amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini
Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa
linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.
Cameron
akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya
unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka
kwa muungano huo wa bara la Ulaya.
0 comments:
Post a Comment