Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema waendesha bodaboda na
abiria wasiovaa helmet watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kutaka
kujiua.
Makonda
aliyemwakilisha Makamu wa Rais kwenye futari iliyoandaliwa na Benki ya
NMB kwa wateja na wadau wake juzi, alisema abiria na wapanda vyombo
hivyo wanatakiwa kuvaa helmet.
Alisema
kupanda pikipiki bila usalama ni kwamba abiria anadhamiria kujiua, kwa
sababu akipata ajali ni rahisi kupoteza maisha kwa kupiga kichwa chini.
“Nimeshawasiliana
na kamati yangu ya usalama barabarani mkoa, hili nitalisimamia
kikamilifu lazima wote wawe na helmet na wakikamatwa wote watashtakiwa,” alisema.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kupanda bodaboda bila kuvaa kofia hiyo, ni sawa na
mtu anayechukua vidonge na kunywa na pombe kali, ambayo matokeo yake ni
kifo.
Makonda
alisema kazi hiyo ataifanya kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani ili
apate thawabu ikiwamo kuruhusu maduka makubwa kufanya kazi hadi usiku wa
manane.
Alisema
hiyo itasaidia wanaofanya kazi wakirudi nyumbani wanafuturu baadaye
wanaswali Tarawehe, hivyo wanaweza kwenda kufanya manunuzi usiku.
Alisema kitakachofanyika ni kuimarisha usalama wa raia kupitia kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Pia, alisema atatangaza kupiga marufuku uvutaji sigara hadharani zaidi kwenye mikusanyiko na kupambana na vijana na watu wanaojihusisha na uvutaji wa shisha (bangi).
Pia, alisema atatangaza kupiga marufuku uvutaji sigara hadharani zaidi kwenye mikusanyiko na kupambana na vijana na watu wanaojihusisha na uvutaji wa shisha (bangi).
“Mtu
asiyevuta sigara, anakerwa sana na moshi ndiye anayeathirika zaidi,
nitatangaza rasmi hivi karibuni marufuku ya kuvuta sigara, sasa watu
watafute kwa kuvutia… nitatangaza na hatua za kuchukua,” alisema.
Makonda alitumia nafasi hiyo kuwataka NMB kuchangia madawati, kwa shule za msingi na sekondari katika mkoa wake.
Makonda alitumia nafasi hiyo kuwataka NMB kuchangia madawati, kwa shule za msingi na sekondari katika mkoa wake.
Awali,
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema utamaduni wa
kufuturu pamoja hasa katika Afrika unadumisha amani, umoja na upendo
miongoni mwa Waislamu na watu wengine, hivyo wao wanauendeleza.
0 comments:
Post a Comment