Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya
Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Prof.
Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake. Prof. Maboko ni
Mhadhiri wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Utaratibu
wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu
kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu
akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu
Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kinyume chake.
0 comments:
Post a Comment