Rich Mavoko, Ommy Dimpoz, Cpwaa, Q-Chief, Chege na Temba ni miongoni
mwa wasanii waliowahi kusafiri na muongozaji wa video, Adam Juma kwenda
kufanya video zao Afrika Kusini.
Na sasa huenda ndoto ya wasanii wengine wenye nia ya kukwea pia na AJ
ili kufanya video zao bondeni huenda zikawa zimefutika rasmi. Ni
kwasababu muongozaji huyo amesema kwa sasa (walau kwa sasa) hana mpango
tena wa kwenda kufanya video zake nchini humo.
“Siwezi kwenda, sasa hivi nina commitment, watoto wanataka kwenda shule. Unalipwa hela ile ile kazi ambayo unaifanya hapa kwa siku moja, it doesn’t make any sense,” aliongeza.
“Mimi nimefanya video nyingi South Africa, lakini nimefanya kwasababu ya kuinvest, lakini sasa ukija kuangalia kwa faida kitu gani tunapata?”
AJ ameendelea kusisitiza kuwa uongozaji wa video kwa Tanzania bado haulipi na hiyo ni sababu iliyomfanya aache kufanya kazi nyingi kama zamani. Amesema kwa sasa atafanya kazi na wasanii ambao wako tayari kumlipa vile anavyotaka au mahitaji muhimu yanayohitajika kufanikisha wazo la video husika.
Hivi karibuni waongozaji wengine wa video nchini wameanzisha utaratibu wa kwenda na wasanii kufanya video Afrika Kusini. Mfano ni video ya Chafu Pozi ya Bill Nass na Pesa ya Madafu ya Jay Moe ambazo zote zilifanyika SA na kuongozwa na Msafiri wa Kwetu Studios.
Waongozaji wanadai kuwa sababu kubwa inayowapeleka Afrika Kusini kufanya video ni upatikanaji rahisi wa location ambapo kwa Tanzania huwawia vigumu kutokana na kutokuwepo utaratibu maalum na huku mamlaka zingine zikiwa na mchakato mrefu wa kuruhusu kutumiwa kwa maeneo husika.
0 comments:
Post a Comment