Real Madrid leo wamethibitisha kumsajili straika wa Juventus Alvaro Morata kwa ada ya paundi milioni 23, wakitekeleza kipengele walichokubaliana wakati wakati wakiwauzia mchezaji huyo miaka miwili iliyopita.
Katika siku za hivi karibuni, Chelsea na Arsenal wamekuwa wakihusishwa na Mhispaniola huyo mwenye miaka 23 huku ripoti mbalimbali zikieleza kuwa Real Madrid watamuuza tena Morata kwa bei ya juu zaidi.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na Real Madrid inaeleza kwamba Zinedine Zidane anamtaka mchezaji huyo kwa ajili ya kumjumuisha katika kikosi cha kwanza kwenye maandalizi ya msimu mpya (pre-season).
Taarifa rasmi iliyotolewa na tovuti ya Real Madrid leo:
“Real Madrid CF imeiarifu Juventus FC juu ya maamuzi ya kutaka kuitumia haki yao katika mkataba wa makubaliano wakati wa kumuuza mchezaji Alvaro Morata, ambaye atajiunga na wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya kwa matakwa ya kocha Zinedine Zidane.”
Gazeti la Marca linaarifu vinginevyo.
Gazeti la Real Madrid Marca linaamini kwamba Real Madrid wanamtaka Morata ambaye walimkuza wenyewe kwenye academy yao ili wamuuze kwa bei ya juu zaidi. Kwa sasa Morata yuko na timu ya taifa ya Uhispania akiiwalisha katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa.
Huku Arsenal na Chelsea zikidaiwa kumnyemelea mchezaji huyo kwa karibu zaidi, Marca linadai kwamba Los Blancos wanataka kuja kumuuza kwa ada ya Euro milioni 75.
0 comments:
Post a Comment