MWENYEKITI
wa kamati ya uchaguzi ya TFF Wakili Aloyce Komba ameamua kujitoa katika
kuratibu na kusimamia mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Yanga uliopangwa
kufanyika tarehe 25 June 2016 na zaidi ametoa sababu 6 zilizomfanya
aamue kujiweka pembeni kwenye mchakato huo.
Sababu zilizomfanya Wakili huyo kuachia ngazi ni kama ifuatavyo;
1.
Katika mchakato huo nimetuhumiwa kupanga kumhujumu kwa kukata jina la
mmoja wa wagombea nafasi ya uenyekiti Bw. Yusuf Manji. Tuhuma ambazo
zilitolewa tarehe 2 June kwa waandishi wa habari.
2.
Kutokana na tuhuma hizo, Yusuf Manji amesema ni moja ya sababu
zilizomfanya achukue fomu za kugombea uchaguzi utakaoratibiwa na Yanga.
3.Tuhuma
hizo ambazo ni kubwa kwangu binafsi na zikigusa taaluma yangu ya sheria
zimetolewa wakati klabu ya Yanga inahitaji amani, utulivu na mshikamano
mkubwa wa wanachama, wapenzi na washabiki wake, hivyo mimi kutokuwa
chanzo chochote cha vurugu zinazoweza kutokea.
4.
Tuhuma hizo zinahusu mimi kupewa fedha za hongo au rushwa (kiasi
hakijulikani) ili nishawishi wajumbe wenzangu wa kamati ya uchaguzi ya
TFF kukata jina la aliyekuwa mgombea mtarajiwa, Bw. Yusuf Manji
kwasababu ambazo hazijaelezwa.
5.
Napaswa kupisha uchunguzi wowote huru wa tuhuma hizo nzito kama
zimeshafikishwa katika vyombo vya uchunguzi wa masuala ya rushwa ili
mimi nipate fursa ya kujitetea kwa uhuru zaidi.
6.Kwa
kuzingatia ushauri wa watu mbalimbali ninaowaheshimu na kuwapenda sana
ndani na nje ya klabu ya Yanga hususani wanasheria wengine nguli wa
masuala ya michezo kama vile Wakili Sais Hamad El-Maamry, Wakili Sam
Mapande, Wakili Alex Mgongolwa na waandishi wa habari waandamizi wa
michezo, nimeona nisishiriki mchakato huu kwa kusimamiwa na TFF au hata
ukisimamiwa na klabu ya Yanga yenyewe.
Kwakuwa
mimi ni muumini mkubwa wa utawala wa sheria na hasa masuala ya katiba
na demokrasia katika vilabu na vyama vya michezo, napaswa kuanzia sasa
kutoshiriki vikao vyote vinavyohusu mchakato wa klabu ya Yanga nikiwa
kama Mwenyekiti au Mjumbe.
Nawaomba
Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi na Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa na
wajumbe wenzangu wa kamati ya uchaguzi ya TFF, nimemuachia madaraka ya
kuratibu na kusimamia uchaguzi wa klabu ya Yanga, Wakili Domina Mideli,
ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo.
0 comments:
Post a Comment