TAARIFA KWA UMMA
Leo
Juni 3/2016 Chama cha ACT Wazalendo Kimeelezea msimamo wake juu ya
uamuzi uliofanywa na Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka ya Bunge
kuwasimamisha wabunge saba wa upinzani akiwemo Mbunge wa ACT Wazalendo
Ndugu Zitto Kabwe.
Uamuzi
huu wa Kamati ya Maadili ambayo sehemu kubwa ya wajumbe wake ni wabunge
wa Chama cha Mapinduzi(CCM) unafuatia msimamo wa wabunge wa upinzani
wakiongozwa na Mbunge wa Chama chetu kupigania maslahi ya wananchi
kupata habari za bunge.
ACT
Wazalendo inaamini Wabunge hawa wametolewa kafara kwa kupinga vikali
uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.
Chama
kimeandaa mapokezi haya yaliyopewa jina maalum la “Opereshen” Linda
Demokrasia, lengo likiwa ni kuwapa nafasi mashujaa waliofukuzwa bungeni
kwa ajili ya kusimamia maslahi ya umma, kuelezea kilichotokea na
kinachoendelea bungeni ambacho watawala hawataki kijulikane.
Pia
katika mkutano wa hadhara Kiongozi wa Chama ndugu Zitto Kabwe
atafafanua kwa kina muktadha wa siasa za sasa na hatari ya kuua vita
dhidi ya ufisadi kutokana na namna demokrasia inavyofifishwa
Kwa
kutambua umuhimu wa utetezi wa maslahi ya wananchi na kuisimamia
serikali kupitia Bunge Chama chetu baada ya mkutano wa Dar esSalaam
utakaofanyika Jumapili ya Juni 5 mwaka huu katika viwanja vya Mbagala
Zakiem, pia Chama kitafanya mikutano mingine mikubwa ya hadhara katika
mikoa ya Mwanza ( 11 Juni, 2016), Kigoma (12 Juni, 2016), Mbeya (18
Juni, 2016) na Morogoro (19 Juni, 2016).
Chama
imeviandikia barua vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi kuviomba
kushiriki kwenye mapokezi hayo.Tunasubiri majibu ya vyama tulivyowaalika
kwa kuwaandikia barua kwa kuwa mpaka sasa hawajatujibu rasmi kama
watashiriki ama la zaidi ya kutufahamisha kuwa wamepokea barua zetu
ACT-Wazalendo,inaamini
“Operesheni Linda Demokrasia” ni muhimu ikapiganwa na vyama vyote
pasipo kujali itakadi ya vyama kwa kuwa hoja hiyo ya kutaka Bunge
lioneshwe moja kwa moja ilipoibuliwa na Mbunge Ndugu Zitto Kabwe kuhoji
hatua ya serikali kubana uwazi Bungeni,wabunge wote wa upinzani
walisimama na kuiunga mkono hoja na kuitetea
Ndugu Ado Shaibu Ado
Katibu, Itikadi Uenezi na Mawasiliano ya Umma,
ACT Wazalendo
0 comments:
Post a Comment