Shirikisho
la Soka Afrika (CAF), limemteua Noiret Jim Bacari wa Comoro kuwa
mwamuzi wa kati katika mchezo wa marudiano utakaozikutanisha timu za
taifa za vijana za Serengeti Boys ya Tanzania na Amajimbos ya Afrika
Kusini, utakaofanyika Agosti 21, 2016 Kwenye Uwanja wa Chamazi ulioko
Mbagala - nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa ya CAF iliyofika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) mapema wiki hii, waamuzi wasaidizi pia wanatoka Comoro. Waamuzi
hao ambao ni washika vibendera ni Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli
wakati mezani atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo
atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir Abdi Hassan.
Jumamosi
iliyopita, ikicheza mbele ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kadhalika Naibu Balozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini, Rosemary Chambe Jairo, timu ya soka ya vijana wenye umri
wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys ilitoka sare ya 1-1 na
Afrika Kusini.
Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko
Kusini – Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana
kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini
ndio walioanza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Luke
Gareth kabla ya Ally Msengi kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika
ya 70.
Penalti
ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys
kumfanyia madhambi Linamandla Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la
hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa
Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa,
William Koto kutoka Lesotho.
Itakumbukwa
kwamba Afrika Kusini ilianza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo
huo, ilipotea dakika zote 30 za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati
na umakini kidogo tu kwa nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa
mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga mwamba hivyo kuwatia hasira
Serengeti Boys ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.
Kubanwa
katika kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos
kufanya mabadiliko ya wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati
Bakari Shime kwa upande wake alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake
kuchukuliwa na Muhsin ambaye alisaidia kuendedlea kuwabana Afrika Kusini
waliokjuwa wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na Lethabo
Mazibuko.
Shukrani
za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari
nyingi ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu
ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema
idarta ya ulinzi akishirikiaana nDickson Job.
Shime
maarufu kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo . Si mabaya
kwangu. Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa inanitia hofu
ndio maana nilisema mechi itakuwa ngumu.”
Kwa
upande wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti
Boys) kwa kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi.
Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya
nchi. Sijui ni nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”
0 comments:
Post a Comment