Saturday, 18 June 2016

ALIYEKUWA BEKI WA TP MAZEMBE ATUA SIMBA.Fahamu zaidi hapa.

Kweli Simba wameamua, tayari beki Janvier Besala Bokungu raia wa DRC, ametua Dar es Salaam kimyakimya ili kumalizana na uongozi wa Msimbazi.
 
Bokungu ni beki wa zamani wa TP Mazembe, kama unakumbuka vizuri ndiye walimchezesha katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikakata rufaa kwenye Shirikisho la Soka Afrika (Caf), TP Mazembe wakaondolewa mashindanoni na Simba kupata nafasi ya kucheza na Wydad Casablanca ya Morocco.
 
 “Tayari wametua hapa nchini na wataanza mazungumzo na taratibu nyingine, maana Bokungu alikuwa Esperance ya Tunisia. Mimi ninaamini atasajiliwa Simba maana kiwango chake kipo juu tu,” kilieleza chanzo.
Caf, ilitangaza uamuzi wa kuiondoa TP Mazembe Mei 14, 2011 na mechi ikachezwa kwenye uwanja huru wa Petrojet jijini Cairo, Misri, Simba ikatandikwa mabao 3-0, hiyo ilikuwa Mesi 28, 2011.
 
 Bokungu yuko jijini Dar es Salaam pamoja  na kiungo mwingine raia wa DR Congo pia wakisubiri ‘kuonwa’ na makocha au watu maalum kabla ya kusaini mkataba kama Simba wataridhika nao.
 
 Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinasema, pamoja na Bokungu na kiungo huyo, mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Blagnon Frederick kutoka Africa Sports ya Ivory Coast alitarajiwa kuwasili jana.
 
 “Kama si jana, basi atatua kesho (leo) tayari kabisa kuanza majaribio na kufanyiwa vipimo kama atakuwa amefuzu,” kilieleza chanzo. Kwa kipindi hiki Blagnon ndiye mfungaji anayeongoza kwa kupachika mabao katika ligi hiyo kwao Didier Drogba.

0 comments:

Post a Comment