June
21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha
taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na
kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote
waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi.
"Jumatatu
ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa
iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani
wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji
mkubwa na wa makusudi kama huu " Amesem a waziri Mwakyembe na kuongeza
"Ukiisoma
taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa
habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa
yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira
wanauhakika ni lini Polisi walinihoji
"Wameona
hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu
kwa kusema kifaru chake cha kivita kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na
kulitia doa jeshi letu. Tukikaa kimya tutaambiwa tena kuwa hicho kifaru
kinatumika kama daladala.
"Tutafungua
kesi hii mahakama kuu ya Tanzania na bado mimi na mawakili wangu
tunaangalia impact na kuhusika kwa vyombo vikubwa vya habari kama ITV
na Star Tv kwa kutangaza taarifa "
0 comments:
Post a Comment