Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>>KESSY ATACHEZA DHIDI YA MAZEMBE? TFF IMETOA UFAFANUZI.Fahamu zaidi hapa.
Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia msemaji wake,
Alfred Lucas limesema kuwa, linashughulikia sakata la uhamisho wa
mchezaji Hassan Kessy Ramadhani kutoka Simba kwenda Yanga ili aweze
kucheza kwenye mchezo wa kimataifa kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe
unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumanne June 28 kwenye uwanja wa taifa.
“Tayari Yanga wameshaandika barua imekuja TFF wakiomba suala la Kessy
liweze kumalizwa haraka ili waweze kumtumia kwenye mchezo wao wa
Jumanne dhidi ya TP Mazembe,”amesema Alfred Lucas afisa habari wa
shirikisho la soka Tanzania.
“Niwahakikishie mashabiki wa Yanga kwamba TFF weekend yote hii kwa
maana ya leo Jumamosi na Jumapili tutalifanyia kazi hilo na tayari
mawasiliano yameshafanyika ili Yanga waanze kumtumia mchezaji huyu mara
baada ya mkataba wake kuisha.”
“Lakini kama kuna kikwazo chochote tunajaribu kufikiria ili Yanaga
wawe huru kusiwe na dosari yeyote kwenye michuano hii halafu sababu
ikawa ni kuwakosa wachezaji wake wote iliyowasajili kwa ajili ya
michuano hiyo.”
“Naamini kwa uungwana waliokuwa nao Simba kama kuna kikwazo
watakiondoa ili mchezaji huyo aendelee kipaji chake na maisha mengine
yaendelee.”
Kessy hakuruhusiwa kucheza kwenye mchezo wa kimataifa kati ya Yanga
dhidi ya MO Bejaia kwasababu kibali chake kutoka Simba kwenda Yanga
kilikuwa hakijathibishwa.
Related Posts:
MABINGWA WA NBA WALIVYOENDA KUMUAGA OBAMA IKULU WAKIONGOZWA NA LeBRON JAMES.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Wachezaji wakipiga selfie mbele ya jengo la ikulu.
Staa
wa kikapu nchini Marekani katika Ligi ya NBA, LeBron James ameiongoza
timu yake ya Cleveland Cavaliers kutembelea ikulu ya nchi hiyo kutokana
na kutwaa ubing… Read More
#MICHEZO>>>>HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOKUTANA NA KIPIGO PALE SOKOINE MBELE YA VIGOGO WAO.FAHAMU ZAIDI HAPA.Timu ya Simba imepoteza mchezo wake
dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa mabao 2-1. Pichani ni matukio
ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulivyochezwa, jana Jumatano.
Viongozi na wadau wa Si… Read More
#MICHEZO>>>>>Azam FC yatoa kichapo kwa Mwadui na kumuenzi Mzee Said vizuri.Fahamu zaidi hapa.
KLABU
Bingwa ya Afrika Mashriki na Kati, Azam FC, jioni ya leo imemuenzi vema
aliyekuwa Mwenyekiti wake, Mzee Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia
juzi jioni, kwa kuipa dozi kali ya mabao 4-1 Mwadui FC katika mche… Read More
#MICHEZO>>>>PLUIJM ASEMA ANAONDOKA YANGA AKIWA BADO ANAIPENDA, ATAIKUMBUKA KWA MENGI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Kocha Hans van der Pluijm amesema ataikumbuka klabu ya Yanga kwa mambo mengi sana kwa kuwa ataondoka akiwa bado anaipenda.
Pluijm raia wa Uholanzi mwenye makazi yake nchini Ghana, amesema Yanga ni moja ya klabu bora kab… Read More
#MICHEZO>>>HECTOR BELLERIN AMDENGULIA GUARDIOLA AJIFUNGA KITANZI KWA WENGER.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Maisha ni safari ndefu ambayo ina
mabonde na milima, wakati matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani
kutangazwa sasa turejee katika michezo na burudani na hapa tunapiga hodi
pale kwa washika bunduki wa London Arsenal ambao … Read More
0 comments:
Post a Comment