RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli ameliagiza jeshi
la Polisi kutumia mbinu za kisasa katika kukabiliana na uhalifu na
kuifanya nchi kuwa sehemu salama nyakati zote.
Dk
Magufuli ameonesha kushangazwa na askari wa Jeshi la Polisi
kunyang’anywa silaha yake na majambazi na wakati mwingine kuuliwa na
majambazi, akihoji uwezo wa majambazi kiasi cha kuwatesa polisi kiasi
hicho.
Rais
alikuwa akizindua Mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao,
ambao una dhamira ya kupunguza uhalifu ambapo ameliagiza jeshi hilo
kuwahi kushughulikia majambazi kabla ya wenyewe kushughulikiwa na
majambazi hayo.
Amesema kama ni silaha
polisi wanazo, mafunzo wanayo lakini wanazidiwa na majambazi hadi
kunyang’anywa silaha kwanini? Pia Rais amelitaka jeshi hilo
kuwashughulikia baadhi ya askari wake ambao hawana nia njema na jeshi
hilo.
Awali
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu alisema mpango huo
unalenga katika maeneo manne akiyataja kuwa ni Kuboresha mbinu
za kupambana na wahalifu na majambazi kwa kuwa na vituo vya polisi vya
kuhamahama na kutumia mfumo wa kisasa wa GPS katika doria za jeshi hilo.
Pili,
Mangu alisema ni kuongeza ubora wa huduma katika vituo vya polisi
ambapo polisi watakuwa wanatatua na kusikiliza kero za wananchi kwa
haraka zaidi na kwa muda mfupi sana.
Tatu
ni kuboresha mawasiliano ndani ya jeshi la polisi pamoja na jamii.
Katika hili IGP Mangu anasema watasaidiwa na mfumo wa GPS katika kuwajua
wananchi wanaosumbua jeshi la Plosi kwa kupiga simu za uongo na zenye
lengo ovu.
0 comments:
Post a Comment