Mkurugenzi
wa Mashitaka Tanzania (DPP), ameiondoa mahakamani rufani aliyoikata
dhidi ya Mawaziri Waandamizi wa zamani, wa Fedha Basil Mramba na wa
Madini Daniel Yona iliyopangwa kusikilizwa jana katika Mahakama ya
Rufani Tanzania.
Rufani
hiyo iliondolewa jana kabla ya kuanza kusikilizwa mbele ya jopo la
majaji watatu likiongozwa na Jaji Mbarouk Mbarouk, Salum Massati na
Profesa Ibrahim Juma.
Mapema
Juni 20, mwaka huu, DPP aliwasilisha kusudio la kuondoa rufani hiyo
chini ya kanuni ya 77(1) ya Mahakama ya Rufani pamoja na nakala
kuwakabidhi mawakili wa utetezi.
Hata
hivyo, jopo hilo lilisema kwamba kifungu alichokitumia DPP kuwasilisha
kusudio hiyo siyo sahihi kwa kuwa kinatumika kabla ya shauri
halijapangwa kusikilizwa.
Jaji
Mbarouk alisema DPP alitakiwa kutumia kanuni ya 4(2)(a) ya Mahakama ya
Rufani kuomba kuondoa rufani hiyo.Mawakili wa Serikali Waandamizi,
Theophil Mutakyawa na Shadrack Kimaro, walieleza nia ya DPP ya kuondoa
rufani hiyo, jambo ambalo halikuwa na pingamizi kwa upande mwingine.
Jopo
hilo lilikubali maombi ya kuondoa rufani hiyo. Mapema mahakamani hapo
DPP alikata rufani kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 2, mwaka 2015 na
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam iliyoketi chini ya Jaji
Projest Rugazia.
Jaji
Rugazia alisema mawaziri hao walitakiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka
miwili na siyo miaka mitatu kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini
Dar es Salaam ilivyowahukumu,dhidi ya mashtaka ya matumizi mabaya ya
madaraka.
Kadhalika,
Jaji Rugazia alikubaliana na hukumu ya kumwachia huru Katibu Mkuu wa
zamani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.
Hata
hivyo, DPP alikata rufani Mahakama Kuu, kupinga adhabu waliyopewa
mawaziri hao kwamba ni ndogo kwa sababu jopo la mahakimu watatu waliotoa
hukumu hiyo walikosea kumwachia huru Mgonja.
Mbali na kupinga adhabu hiyo, DPP aliomba mahakama kuwaamuru washtakiwa kulipa fidia ya fedha walizosababisha hasara.
Mahakama
ya Kisutu, iliwahukumu Mramba na Yona kutumikia kifungo cha miaka
mitatu jela na kulipa faini ya sh. milioni tano, baada ya kupatikana na
hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya
sh. bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya
kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
Kwa
sasa mawaziri hao wanatumikia kifungo cha nje baada ya kupendekezwa
kuwa miongoni mwa wafugwa wanaohitaji kumalizia sehemu ya kifungo chao
wakiwa nje, ikiwamo kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina.
0 comments:
Post a Comment