Kauli
ya Rais ya Kuzuia Vyama vya Siasa Kufanya Shughuli za Siasa kwa Miaka
Mitano ni Tangazo la Vita dhidi ya Demokrasia na Mfumo wa Vyama vingi
Nchini
Tumepokea
kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa
havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni.
Kimsingi
kauli ya Rais ni kauli yenye nia ya kuvunja Sheria ya Vyama vya siasa
inayolinda uwepo wa mfumo wa vyama vingi na kuhimiza vyaMA vya siasa
kufanya shughuli za siasa katika msimu wote ili kuthibitisha uhai wao.
Tunaichukulia
kauli ya Rais kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama
vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya
siasa nchini na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea
dhidi ya demokrasia nchini mwetu.
Tunatoa
wito kwa vyama vyote vya siasa vinavyoamini katika misingi ya
demokrasia nchini kukutana haraka na kujadili namna ya kuunganisha nguvu
pamoja katika kupigana vita mpya ya kulinda demokrasia nchini mwetu.
Aidha,
tunatoa wito kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara
katika kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi
duniani kote unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za
maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini
mwetu.
Hatua
zozote za kuua demokrasia ni kuua Umoja, Amani na Mshikamano wa
wananchi na Taifa, ambayo ndiyo misingi ya maendeleo ya nchi yetu
kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Tunatoa wito kwa wananchi wote kushikamana na kusimama imara katika kipindi hiki kigumu ili kulinda demokrasia.
Zitto Kabwe, MB
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Alhamisi, 23 Juni 2016.
0 comments:
Post a Comment