Wanaharakati
na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni
aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akalipe faini
aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu.
Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa facebook.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Mratibu
aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini, Diwani wa
Levolosi, Ephata Nanyaro amesema jana kuwa wamefanikiwa kupata
michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha.
"Lengo
ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini
hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, " amesema Nanyaro.
Naye,
Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia akisema
kupitia adhabu hiyo atakuwa wa kwanza kufundisha jamii kuhusu sheria za
mitandaoni.
0 comments:
Post a Comment