Uzimaji wa Imei bandia ulifanyika usiku wa kuamkia jana kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika simu zaidi ya 600,000 zenye Imei batili.
Kwa mujibu wa
TCRA, Imei ni namba ya kimataifa ya utambuzi wa vifaa vya kielektroniki,
ikiwamo simu. Ina tarakimu 15 ambazo ni za kipekee kwa kifaa husika na
zinatambulika kimataifa. Namba hizo hutumika kudhibiti bidhaa bandia au
simu kutumiwa na mtu mwingine.
Jana,
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema
takwimu hizo ni zile ambazo zimetokana na kazi ya kukata mawasiliano
katika simu bandia iliyofanyika kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi
alfajiri ya jana.
Alisisitiza kuwa mtambo huo unaendelea na kazi
kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazipo au hazikuwa hewani
zitakapowashwa hazitafanya kazi.
“Kazi ya kuzima simu hizo ilianza usiku
wa kumkia jana saa sita usiku na kila kampuni ya mtandao wa simu
ilipaswa kuzima simu za wateja wake ambazo ni feki na kazi ya mtambo ni
kuhakikisha simu iliyozimwa inapowekewa kadi ya mtandao mwingine
haifanyi kazi na kuhakikisha simu zote feki zitakazoingia nchini
hazifanyi kazi,” alisema Mungy.
Hata hivyo, kuna baadhi ya wamiliki wa
simu ambao walitilia shaka ufanisi wa mtambo huo kwa madai kuwa tayari
walishathibitishiwa na TCRA kwamba simu zao ni feki, lakini bado
zinafanya kazi.
“Simu yangu mimi niliangalia nikaambiwa ni feki na
niibadilishe kabla ya tarehe 16 Juni, lakini jana wamezizima feki ya
kwangu bado inafanya kazi kama kawaida napiga na kupokea simu kama
zamani,” alisema Nael Joseph.
Kuhusu suala hilo, Mungy alisema: “Hoja hizo zimejitokeza kwa wingi na wengine walifikia hatua ya kuushutumu mtambo wetu kuwa ni feki na kuwa umeshindwa kuzima simu feki ukazima orijino, lakini ukweli ni kwamba mtambo ule hauzimi kama taa au kama ule uliozima matumizi ya analojia bali unazima taratibu.
"Niweke sawa kwamba mtambo huu hauonei mtu na unazima simu zote zilizo feki.”
Mungy aliongeza kuwa wengi wamekuwa hawaelewi mantiki ya ujumbe wa uthibitisho.Alisema ujumbe unamtaka mmliki wa simu kuoanisha jina linalotajwa kama ndilo jina halisi la simu yake. “Kama jina linalotajwa na Imei linaoana na lililoandikwa kwenye simu yako, basi sio feki, lakini majina yakiwa hayafanani ndipo simu inakuwa feki,” alifafanua.

Vodacom wazungumza
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom, Rosalynn Mworia alisema walipewa
jukumu la kuzima simu feki za wateja wao na TCRA.
“Jana saa sita usiku
tulitekeleza agizo kama lilivyotolewa na TCRA na inavyoonekana wengi
wao walikuwa wamejipanga kwani simu nyingi zimezimwa, lakini baadhi
wamerejea hewani japokuwa wapo ambao mpaka sasa hawajarudi,” alisema
Mworia .
0 comments:
Post a Comment