Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limetuma timu ya maofisa wake kwenda mikoa ya Arusha na Mwanza kufanya upelelezi wa mauaji ya dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.
Hadi
sasa jeshi hilo limewakamata watu wanne kwa tuhuma za mauaji hayo,
akiwamo mumewe Aneth, mfanyakazi wao wa ndani na hawara wa mfanyakazi
huyo.
Kamanda Sirro hakumtaja mtuhumiwa wa nne aliyekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo yaliyogusa hisia za watu.
Aneth
aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojuliana Mei 26 mwaka huu, nyumbani
kwake Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao inadaiwa hawakuchukua
kitu chochote ndani na kutoweka.
Sirro alisema alituma maofisa hao kwenda Mwanza na Arusha kufanya upelelezi wa mauaji ya Aneth ili kubaini chanzo chake.
Hata
hivyo, hakutaka kufafanua zaidi sababu za kutuma timu hiyo kwenye mikoa
hiyo wakati mauaji hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam.
“Jeshi la polisi bado tunafuatilia, kwa sasa tumeshatuma maofisa wetu wameenda katika mkoa wa Mwanza na Arusha ili kufanya upelelezi zaidi,”alisema Sirro.
“Jeshi la polisi bado tunafuatilia, kwa sasa tumeshatuma maofisa wetu wameenda katika mkoa wa Mwanza na Arusha ili kufanya upelelezi zaidi,”alisema Sirro.
Alisema
jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa wanaowashikilia ili kubaini
chanzo cha mauaji hayo, hivyo upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani.
Bilionea
Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 12 na watu wanaosadikiwa kuwa
majambazi kandokando ya barabara eneo la Mojohoroni wilayani Hai Mkoa
wa Kilimanjaro.
Februari
10, mawakili wanaosimamia kesi ya bilionea huyo, Hudson Ndusyepo,
Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu, waliiambia mahakama kuwa
Serikali inakusudia kuita mashahidi 50 kuthibitisha mashtaka na
kuwasilisha vielelezo 40, ikiwamo bunduki iliyotumika katika mauaji
hayo.
Mawakili
hao walidai mipango ya kumuua bilionea Msuya ilianza Julai 26, mwaka
2013 jijini Arusha, ikiwahusisha washtakiwa hao baada ya kuahidiwa
wangelipwa Sh5 milioni kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment